Milima ya Kipengere

Mandhari ya milima ya Kipengere na misitu yake.

Milima ya Kipengere (kwa Kiingereza: "Kipengere Range" au "Livingstone Mountains") iko kusini magharibi mwa Tanzania kwenye ncha ya kaskazini ya Ziwa Malawi.

Milima yake ya kaskazini inaitwa pia Milima ya Poroto[1] na ile karibu na ziwa inaitwa pia Milima ya Ukinga.

Ni safu ya milima inayoelekea kusini mashariki kutoka bonde la mto Ruaha Mkuu upande wa kaskazini hadi lile la mto Ruhuhu upande wa kusini kwa kufuata Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Kilele chake ni Mlima Jamimbi unayoshuka moja kwa moja ziwani.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  1. MSN Encarta World Atlas. Retrieved 19/9/07.

Majiranukta kwenye ramani: 9°30′S 34°10′E / 9.5°S 34.167°E / -9.5; 34.167