Mohamed Ould Abdel Aziz

Mohamed Ould Abdel Aziz (kwa Kiarabu: محمد ولد عبد العزيز‎ Muḥammad Wald ‘Abd al-‘Azīz; amezaliwa 20 Desemba 1956) ni mwanasiasa wa Mauritania ambaye alikuwa Rais wa 8 wa nchi, madarakani kutoka mwaka 2009 hadi 2019.

Mohamed Ould Abdel Aziz August 2014 (cropped).jpg

Askari kwa kazi na afisa wa ngazi ya juu, alikuwa kiongozi wa mapinduzi ya Agosti 2005 ambayo yalimuondoa Rais Maaouya Ould Sid'Ahmed Taya, na mnamo Agosti 2008 aliongoza mapinduzi mengine, ambayo yalimpindua Rais Sidi Ould Cheikh Abdallahi.

Kufuatia mapinduzi ya 2008, Abdel Aziz alikua Rais wa Halmashauri Kuu ya Nchi kama sehemu ya kile kilichoelezwa kama mpito wa kisiasa unaoandaa uchaguzi mpya. Alijiuzulu wadhifa huo mnamo Aprili 2009 ili kusimama kama mgombea katika uchaguzi wa rais wa Julai 2009, ambao aliushinda. Aliapishwa mnamo 5 Agosti 2009. Alichaguliwa tena mnamo 2014, halafu hakutaka kuchaguliwa tena mnamo 2019. Alibadilishwa na Mohamed Ould Ghazouani, ambaye alichukua madaraka tarehe 1 Agosti 2019.

Abdel Aziz pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kutoka 2014 hadi 2015.

Crystal personal.svg Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mohamed Ould Abdel Aziz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.