Money Mondays
"Money Monday" ni jina la albamu ya kwanza kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Vanessa Mdee. Albamu imetoka rasmi tarehe 15 Januari, 2018, japo utangazaji wake ulianza tangu Novemba na mnamo tarehe 29 Disemba 2017 aliita vyombo vya habari kwa ajili ya utambulisho na uzinduzi huku akisindikizwa na Mohombi kutoka Sweden.[2] Januari 20, 2018 alikutana na mashabiki wake pale Mlimani City na kuwauzia albamu hii huku akitia saini katika kava za albamu. Baadaye Jux akaja na kununua albamu 25 kuahidi kuzigawa kwa watu wake wa karibu.[3] Albamu ina jumla ya nyimbo 18, huku 2 zikiwa kama nyimbo za ziada. Albamu imetayarishwa na watayarishaji mbalimbali lakini kazi kubwa ya kuiboresha ilifanywa na Chizan Brain kupitia B. Records. Nyimbo zilizotolewa kama singo ni pamoja na Cash Madame, Kisela na Bounce. Nyimbo zilizowekwa kama za ziada ni pamoja na No Body But Me aliyoimba na KO na Juu aliyoimba na Jux.[4]
Wasanii walioshirikishwa kutoka katika albamu ni pamoja na Mohombi kutoka Sweden, Konshens kutoka Jamaica, Cassper Nyovest na K.O wote kutoka Afrika Kusini. Wengineo ni kina Joh Makini, Mr P, Reekado Banks, G Nako, Tahpha, Tammy Flavor, Maua Sama na Jux. Kwa upande wa utayarishaji albamu kuna mkono wa Nahreel, Kelly, S2Keezy, Tahpha, Bob Manecky, Breezy na Lufah.
Money Mondays | ||
---|---|---|
Studio album ya Vanessa Mdee | ||
Imetolewa | 15 Januari, 2018[1] | |
Imerekodiwa | 2015, 2016-2017 | |
Aina | R&B, muziki wa dunia, ragga dancehall, Bongo Flava | |
Lebo | Mdee Music | |
Mtayarishaji | Vanessa Mdee (Mtayarisha Mkuu) Nahreel Ekelly S2keezy Tahpha Bob Manecky Breezy Elloriks Music Lufa |
|
Single za kutoka katika albamu ya Money Mondays | ||
|
Historia
haririMazungumzo juu ya albamu yalianza miaka mingi. Lakini tarehe19 Aprili, 2015, Vanessa alifunguka kiasi kuhusu jina la albamu na nia ya kuita hivyo katika kipindi cha "The Playlist" cha Times FM - katika mahojiano yake na Lil Ommy. Nessa alisema kwa vile wanamwita Vee Money, na alitaka kutengeneza albamu ambayo itaelezea pilika zake za muziki tangu alikotoka hadi sasa. Hasa ukitazamia Monday ni siku ya kwanza katika wiki za kazi, na kila mtu huenda mihangaikoni kujitafutia riziki.[5] Yeye hasa aliona kila Jumatatu, yaani, Monday, ni fursa mpya katika kubadilisha maisha yako. Halkadhalika imetumika kama sitiari ya kutokata tamaa, kwani ikiwa umekosa Jumatatu iliyopita, basi Jumatatu hii ile fursa unaweza kujaribu tena na tena. Nessa, anaona safari yake ya kimuziki inaanza rasmi baada ya kutoa albamu. Katika mahoajiano hayo, alitaja baadhi ya nyimbo zitakazo kuwepo katika albamu. Nyimbo hizo ni pamoja na Closer, No Body But Me, Come Over, Siri na Hawajui. Lakini baada ya kutoka albamu nyimbo zilizotajwa hazikuwepo zote, bali moja tu "No Body But Me". Nayo iliwekwa kama wimbo wa ziada ikiwa imeongozana na "Juu" ambayo kaimba na mpenzi wake Juma Jux.
Ili kutimiza jina la albamu, karibia nyimbo nyingi za Nessa zimetolewa siku ya Jumatatu, yaani, Monday. Nyimbo hizo ni pamoja na Kisela, Hawajui, na albamu imetolewa tarehe 15 Januari, 2018 nayo ni Jumatatu. Vilevile mapato atakayopata kupitia wimbo wa "Pumzi ya Mwisho" atagawana nusu kwa nusu na familia ya Mbaraka Mwinshehe. Nessa kabla ya kutoa albamu, aliiendea familia ya marehemu Mbaraka Mwinshehe na kuomba ridhaa ya kutumia sehemu ya kionjo cha nyimbo hiyo. Gawio kwa familia hiyo ni kwa manunuzi ya kidijitali, yaani uuzwaji kwa njia ya mtandaoni.[6]
Orodha ya nyimbo
haririHii ni orodha ya nyimbo zinazopatikana katika albamu ya "Money Mondays".
Na. | Jina la wimbo | Mtayarishaji | Maelezo |
---|---|---|---|
1 | Intro | ||
2 | Kisela | Ekelly | Kamshirikisha Mr. P wa P Square. |
3 | Unfollow | S2keezy | |
4 | Floating On a Wave | Nahreel | |
5 | Don’t You know | Nahreel | Akiwa na Tahpha |
6 | African Hustle | (Interlude) | |
7 | Cash Madame | Ekelly | |
8 | Pumzi ya Mwisho | S2keezy | Kamshirikisha Cassper Nyovest na Joh Makini |
9 | Wet | Nahreel | akiwa na G Nako |
10 | Scratch My Back | Elloriks Music | Radio na Weasel |
11 | Shadee | (Interlude) | |
12 | Bounce | Breezy | Maua Sama na Tommy Flavour |
13 | Kwangu Njoo | Breezy | Akiwa na Mohombi |
14 | The Way You Are | Bob Manecky | |
15 | Bomb | Nahreel | akiwa na Konshens |
16 | Bambino | Ekelly | Akiwa na Reekado Banks |
17 | No Body But Me | Nahreel | Akiwa na KO |
18 | 18. Juu | Lufa | Akiwa na Jux |
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ Nyimbo za album ya ‘Money Mondays’ ya Vanessa Mdee zatajwa Bongo5 ingizo la 21-12-17
- ↑ Nessa Mlimani City Millard Ayo, mnamo tarehe 29.12.2017
- ↑ JUX amwaga mahela kwa Vanessa avunja record kwa kununua CD 25 Mlimani City Millard Ayo, Youtube mnamo 20 Januari, 2018.
- ↑ Vanessa Mdee – Money Mondays (Album Tracklist) Archived 28 Januari 2018 at the Wayback Machine. DJ Mwanga, Disemba 2017.
- ↑ VANESSA MDEE anaichambua album yake ya MONEY MONDAYS LIVE On AIR: kwenye idhaa ya Lil Ommy huko YouTube, mnamo 23 Januari, 2018.
- ↑ Albamu ya Vanessa Mdee kuinufaisha familia ya Mbaraka Mwishehe Gazeti la Mwananchi, 20 Januari, 2018.