Nahreel

Mwanamuziki & mtayarishaji wa muziki

Emmanuel Mkono (alizaliwa 12 Desemba 1989 jijini Dar es Salaam), anajulikana kwa jina la kisanii Nahreel, ni msanii wa Kitanzania wa kurekodi midundo ya Afro/ Dancehall na mtayarishaji wa rekodi. Yeye ndiye mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa sasa wa The Industry Studios. Nahreel ni mwanzilishi mwenza na mwanachama wa kundi la muziki la Navy Kenzo. Ametayarisha albamu na kusimamia kazi za rappers na waimbaji wengi, akiwemo Vanessa Mdee, Joh Makini, Diamond Platnumz, Nikki wa pili, Navy Kenzo, Izzo Biznes, Gnako, K.O, Roma Shrekeezy.,[1] Anatajwa kuwa ni mhusika mkuu katika kueneza rap ya Kiingereza nchini Tanzania.

Nahreel
Jina Kamili Emmanuel Mkono
Jina la kisanii Nahreel
Nchi Tanzania
Alizaliwa 12 Desemba 1989
Aina ya muziki Dancehall,Rap
Kazi yake Mwanamuziki
Miaka ya kazi 2008 - hadi leo

Maisha yake ya awali

hariri

Nahreel alipendezwa na muziki akiwa na umri wa miaka 14 baba yake alipomnunulia piano na mwalimu wa kumfundisha jinsi ya kucheza. Alianza rasmi taaluma ya muziki akiwa mtayarishaji msaidizi wa muziki katika studio ya Kama Kawa Records jijini Dar es Salaam. Alifanya kazi huko kwa muda wa miaka miwili kabla ya kuondoka kwenda India kuendeleza masomo yake katika Chuo cha Punjab. Ala yake ya Riz One aliyoipigia Izzo Bizness iliyotoka chini ya MJ Records ilimfanya rapa Izzo Bizness kuwa miongoni mwa wasanii wa Tanzania waliofanya vizuri zaidi mwaka 2009. Pia ala hiyo ilimfanya Nahreel kupata nomination za tuzo kubwa na kukutana na mtoto wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Rithiwan Kikwete. Alikuwa bado India kwa wakati huu lakini hitaji la ala zake lilikuwa kubwa nchini Tanzania kwani wasanii wengi wa hip-hop walipenda kufanya kazi naye.[2],[3]

Mwaka 2011, alimaliza elimu yake nchini India na kurejea Tanzania. Alitoa nyimbo kadhaa kabla ya kujiunga na marafiki zake kadhaa kuunda kikundi cha muziki cha Pah One.

The Industry

hariri

Mnamo Agosti 2014, Nahreel alifungua kampuni yake inayoitwa The Industry. Sekta hii inajumuisha studio za The Industry (lebo, mahusiano ya umma, usimamizi) na Industry School Of Music. Sekta hiyo tangu wakati huo imefanya kazi kwenye miradi mingi mikubwa na kampuni kubwa tofauti na wasanii. Lebo ya The Industry iliwahi kusimamia wasanii wawili akiwemo Wildad na rapa wa kike, Rosa Ree.

Hizi ni tuzo alizoshiriki au kupokea kutoka WatsUp TV Africa Music Video Awards.[4]

Mwaka Mteule / kazi Tuzo Matokeo
2016 Kamatia Video Bora ya Reggae Dancehall Alichaguliwa [5]
2016 Kamatia Video Bora ya Kikundi Alishinda

Nyimbo

hariri
  • Stimu zimelipiwa - Joh Makini (2010) (ilishinda kili awards wimbo bora wa hip hop wa mwaka)
  • Tanzania - Roma (2008)
  • Tanzania - Kala Jeremiah (2008)
  • Niaje ni vipi - Joh ft Nikki II (2008)
  • Mziki huu - Izzo Bizness (2008)
  • Nakabaa koo - Izzo Bizness (2008)
  • Kiujamaa - Nikki II (2011)
  • RiziOne - Izzo Bizness (2011)
  • Ghetto - Pah One (2012)
  • Amatita - Pah One (2011)
  • You - Pah One (2011)
  • I wanna get paid - Pah One (2012)
  • Kuwa na Subira - Rama Dee (2012)
  • Zawadi - Vinega (Anti-Virus) (2012)
  • Kila kitu nyerere - Bonta (2011)
  • Usinibwage - Aika and Nahreel (2013)
  • Come Over - Vanessa Mdee (2013)
  • Chelewa - Navy Kenzo (2013)
  • Nje ya Box - Nikki II ft Joh Makini and Gnakko (2013)
  • Gere - Weusi (2014)
  • Namchukua - Shilole (2014)
  • Naogopa - Gosby ft Ommy Dimpoz(2014)
  • Kolo kolo - Mirror (2014)
  • Sukido - Quick Racka ft Barnaba (2014)
  • Malele - Shilole (2014)
  • Hamjui - Vanessa Mdee (2014)
  • Aiyola - Navy Kenzo (2014)
  • Switch on Jingle - Airtel Tanzania (2014)
  • Safari - Nikki wa pili ft Johmakini, Vanessa Mdee, Jux, Aika & Nahreel (Navy Kenzo) (2014)
  • Moyoni - Navy Kenzo (2014)
  • I just wanna love you - Navy kenzo (2014)
  • Nobody but me - Vanessa Mdee ft KO (2015)
  • Nusu Nusu - Joh Makini (2015)
  • Nana - Diamond Platnumz ft Mr Flavour (2015)
  • Zigo - Ay (2015)
  • Mfalme - Mwana FA ft Gnakko (2015)
  • Game - Navy Kenzo ft Vanessa mdee (2015)
  • Looking for you - Jux (2015)
  • Laini - Gnakko ft Nikki wa Pili (2015)
  • Zigo(Remix) Ay ft Diamond Platnumz
  • Kamatia - Navy Kenzo
  • Never ever -Vanessa Mdee. Waya 2016- Weusi
  • Navy Kenzo - Fella

Marejeo

hariri
  1. "Nahreel biography: wife, parents, net worth, songs, facts". Tuko (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-08-05.
  2. "Nahreel breaks silence on cheating allegations". The Citizen (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-11.
  3. "Mr Gold welcome to the world- Navy Kenzo's Nahreel and wife Aika welcome new born son". The Citizen (kwa Kiingereza).
  4. https://web.archive.org/web/20170117120711/http://www.wazobiaforum.com/post/24957/yemi-alade-wizkid-cassper-diamond-rihanna-shatta-wale-nominated-for-2016-watsup-tv-africa-music-video-awards
  5. https://web.archive.org/web/20170117111407/https://www.monteoz360.com/2016/10/wamva2016-full-nominees-list-of-2016-watsup-tv-africa-music-video-awards
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nahreel kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.