Uswidi
Uswidi (kwa Kiswidi: "Sverige") ni nchi ya Skandinavia katika Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Ufini (Finland) na Norwei.
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: För Sverige i tiden1 (Kiswahili: "Kwa Uswidi, wakati wake") | |||||
Wimbo wa taifa: Du gamla, du fria ("Wewe kizee,wewe huru") | |||||
Mji mkuu | Stockholm | ||||
Mji mkubwa nchini | Stockholm | ||||
Lugha rasmi | Kiswidi2 | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba Carl XVI Gustaf Magdalena Andersson | ||||
Kuungana kwa nchi {{{established_events}}} |
{{{established_dates}}} | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
450,295 km² (55) 8.7% | ||||
Idadi ya watu - 2021 kadirio - 2013 sensa - Msongamano wa watu |
10,402,070 (2021) (88) 9,658,301 25/km² (198) | ||||
Fedha | Swedish krona (SEK )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) | ||||
Intaneti TLD | .se | ||||
Kodi ya simu | +46
| ||||
1 För Sverige i tiden ni kaulimbiu ya mfalme Carl XVI Gustaf 2 Kiswidi ni lugha ya kitaifa kuanzia mwaka 2009. Lugha nyingine tano zimekubalika rasmi kama lugha za vikundi vidogo ndani ya taifa. |
Jiografia
haririNchi imegawiwa katika mikoa mitatu: Norrland katika kaskazini, Svealand katikati na Götaland katika kusini.
Ina pwani ndefu kwenye bahari ya Baltiki. Kuna daraja la kuvukia mlango wa bahari ya Oresund ya kuunganisha Uswidi na Denmark.
Kuna misitu mikubwa sana na maziwa mengi.
Hali ya hewa ya sehemu kubwa ya Uswidi si baridi kutokana na athira ya mkondo wa Ghuba. Kuna tofauti kati ya urefu wa mchana katika miezi ya Mei hadi Julai na giza wakati wa Desemba. Tarehe 21 Juni ni siku ndefu: hakuna giza kabisa na usiku wake Waswidi hufanya sherehe kubwa ya "midsommar" kwa ngoma na dansi kote nchini.
Mji mkuu ni Stockholm, nao unaongoza kwa wingi wa wakazi.
Milima na vilele
haririVilele vya juu kwa kila "landskap" ni kama ifuatavyo. Kumbuka kwamba "landskap" katika Uswidi ni sahihi kidogo tu. Basi maoni mengine kuwepo.
Landskap | Mlima | Kimo |
---|---|---|
Blekinge | Rävabacken | 189 |
Bohuslän | Björnerödspiggen | 222 |
Dalarna | Storvätteshågna | 1204 |
Dalsland | Baljåsen | 302 |
Gotland | Lojsta hed | 83 |
Gästrikland | Lustigknopp | 402 |
Halland | Högalteknall | 226 |
Hälsingland | Garpkölen | 671 |
Härjedalen | Helags | 1797 |
Jämtland | Storsylen | 1743 |
Lappland | Kebnekaise | 2104 |
Medelpad | Myckelmyrberget | 577 |
Norrbotten | Vitberget | 594 |
Närke | Tomasbodahöjden | 298 |
Skåne | Söderåsen | 212 |
Småland | Tomtabacken | 377 |
Södermanland | Skogsbyås | 124 |
Uppland | Tallmossen | 118 |
Värmland | Granberget | 701 |
Västerbotten | Åmliden | 550 |
Västergötland | Galtåsen | 361 |
Västmanland | Fjällberget | 466 |
Ångermanland | Tåsjöberget | 635 |
Öland | Högsrum | 55 |
Östergötland | Stenabohöjden | 328 |
Wilaya
haririLän | Herufi | Mji mkuu | Eneo | Ramani |
---|---|---|---|---|
Blekinge län | K | Karlskrona | 2.947 km² | |
Dalarnas län | W | Falun | 28.196 km² | |
Gotlands län | I | Visby | 3.151 km² | |
Gävleborgs län | X | Gävle | 18.200 km² | |
Hallands län | N | Halmstad | 5.462 km² | |
Jämtlands län | Z | Östersund | 49.343 km² | |
Jönköpings län | F | Jönköping | 10.495 km² | |
Kalmar län | H | Kalmar | 11.219 km² | |
Kronobergs län | G | Växjö | 8.467 km² | |
Norrbottens län | BD | Luleå | 98.249 km² | |
Skåne län | M | Malmö | 11.035 km² | |
Stockholms län | AB | Stockholm | 6.519 km² | |
Södermanlands län | D | Nyköping | 6.103 km² | |
Uppsala län | C | Uppsala | 8.208 km² | |
Värmlands län | S | Karlstad | 17.591 km² | |
Västerbottens län | AC | Umeå | 55.190 km² | |
Västernorrlands län | Y | Härnösand | 21.685 km² | |
Västmanlands län | U | Västerås | 5.145 km² | |
Västra Götalands län | O | Göteborg | 23.956 km² | |
Örebro län | T | Örebro | 8.546 km² | |
Östergötlands län | E | Linköping | 10.645 km² | |
Jumla | 410.977 km² |
Historia
haririWakazi wa kwanza kujilikana walikuwa makabila ya Kigermanik kama wakazi wote waliowafuata. Huko Roma Tacitus aliandika juu yao mwaka 98 BK.
Kati ya karne ya 8 hadi ya 11 waliitwa mara nyingi "Waviking" wakiogopwa na wenyeji wa Ulaya bara kwa sababu Waviking walivamia mara kwa mara maeneo ya pwani kwa jahazi zao ndogo. Lakini Waviking au Wanormani ni neno la kutaja watu wa Kaskazini waliovamia na kufanya ujambazi kwenye nchi za Ulaya bara si namna jinsi wenyewe walivyojiita.
Malkia Margarete I wa Udani aliolewa na mfalme wa Norway. Baada ya kifo cha mumewe alitawala nchi zote mbili na baadaye pia Uswidi. Mwaka 1397 wawakilishi wa falme tatu zilikutana katika mji wa Kalmar (Uswidi ya kusini) na kuelewana juu ya "Umoja wa Kalmar" yaliyounganisha nchi zote za Skandinavia chini ya mfalme wa Denmark ilhali kila nchi iliendelea kujitawala. Wakati ule Ufini (Finland) ilikuwa chini ya Uswidi. Iceland na Visiwa vya Faroe ziliingia pia kwa sababu zilikuwa chini ya Norway wakati ule.
Umoja huo uliendela hadi mwaka 1521. Waswidi walianza kuchoka na utawala wa Kidenmark wakaondoka katika umoja huu mwaka 1521 pamoja na Ufini. Lakini Norway iliendela kuwa chini ya Denmark hadi mwaka 1814.
Uswidi ulijiunga na Matengenezo ya Kiprotestanti na kanisa la Kilutheri likawa dini rasmi nchini hadi mwaka 2000. Hivyo Uswidi ikawa kati ya nchi muhimu sana ya Ulutheri.
Uswidi ulistawi na kueneza himaya yake kuanzia karne ya 17 hadi mwanzo wa karne ya 18 kama mojawapo kati ya nchi zenye nguvu zaidi Ulaya.
Baadaye ilirudi nyuma hadi kunyang'anywa kwa Ufini na Warusi (1809).
Kati ya miaka 1814 na 1905 ililazimisha Norwei kukubali mfalme wa Uswidi kama mfalme wa Norwei pia.
Tangu hapo Uswidi umeshika msimamo wa amani na wa kutoshikamana na nchi yoyote.
Kwa sasa Uswidi ni ufalme wa kikatiba yaani Mkuu wa Dola ni mfalme (kwa sasa Carl XVI Gustaf), lakini huyu mfalme anapaswa kufuata sheria ya katiba ya nchi. Utawala umo mikononi mwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia.
Katika karne ya 20 Uswidi umefaulu vizuri kujenga uchumi ili kuondoka katika umaskini na kuwa moja kati ya nchi tajiri za dunia (ikiwa na nafasi ya 8 kwa pato la kichwa).
Nchi ilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 1995 lakini haikukubali pesa ya Euro ikaendelea na Krona ya Uswidi.
Watu
haririUswidi ni nchi kubwa yenye wakazi wachache: mwaka 2017 kwa mara ya kwanza wamezidi milioni 10, wengi wao wenye asili ya makabila ya Kijerumani, lakini kwa sasa 32.2% wana damu tofauti au mchanganyiko.
Lugha rasmi ni Kiswidi, ambacho kinafanana sana na Kidani na Kinorwe. Lugha ya pili kati ya tano zilizokubalika kwa makundi madogo ya asili ni Kifini (5%), lakini siku hizi uhamiaji umefanya Kiarabu kiwe na watumiaji wengi zaidi.
Asilimia 89 wanaweza kuongea Kiingereza pia.
Upande wa dini, 57.7% ni Walutheri, lakini kati yao 2% tu wanashiriki ibada ya kila wiki. Waprotestanti wengine ni 275,000, Waorthodoksi wa Mashariki 100,000 na Wakatoliki 92,000.
Waislamu ni kama 600,000, lakini wengi hawashiriki, na 25,000 tu wanafuata swala tano.
Picha
hariri-
Kebnekaise ni mlima mkubwa wa Uswidi
-
Ziwa la Vänern
-
Wanyamapori wakubwa wa Uswidi ni mbawala wakubwa
-
Stockholm – mji wa kale
-
Migodi ya Kiruna
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Sweden entry at The World Factbook
- Sweden entry at Encyclopædia Britannica
- Sweden Archived 25 Januari 2009 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Uswidi katika Open Directory Project
- Sweden profile from the BBC News
- Wikimedia Atlas of Sweden
- Key Development Forecasts for Sweden from International Futures
- Study in Sweden – Official guide to studying in Sweden
- [1] Archived 30 Desemba 2014 at the Wayback Machine. Technological Waves and Economic Growth in Sweden 1850–2005
- Sweden – Economic Growth and Structural Change, 1800–2000 — EH.Net Encyclopedia
- vifanord – A digital library that provides scientific information on the Nordic and Baltic countries as well as the Baltic region as a whole
- Tovuti rasmi
- Sweden.se — Sweden's official portal
- The Swedish Parliament – Official website
- The Government of Sweden – Official website
- The Royal Court Archived 11 Oktoba 2016 at the Wayback Machine. – Official website of the Swedish Monarchy
- Habari
- Radio Sweden – Public service
- Sveriges Television (Kiswidi) – Public service
- Dagens Nyheter (Kiswidi)
- Svenska Dagbladet (Kiswidi)
- The Local – Sweden's news in English – Independent English language news site
- Biashara
- Utalii
- VisitSweden.com – Official travel and tourism website for Sweden
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uswidi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |