Monika Fornaçon
Monika Fornaçon (alizaliwa Februari 2, 1964), alikua mwamuzi wa mpira wa miguu wa Ujerumani. [1]
Kazi
haririKama mchezaji
haririMnamo 1978 hadi 1991 Fornaçon alicheza mpira wa miguu huko Steimbke na Haßbergen .
Kama mwamuzi
haririMnamo 1981 alikua kaimu mwamuzi. Mwaka 1991 hadi 2004 alisajiliwa katika orodha ya Shirikisho la Soka la Ujerumani, 1998 hadi 2003 katika orodha ya FIFA . Mwaka 2000 alichezesha fainali ya kombe la wanawake la DFB-Cup huko Berlin . Alichezesha mechi kadhaa za kimataifa na vile vile katika mashindano ya UEFA ya wanawake 2001 nchini Ujerumani . Fornaçon pia alikubaliwa kuwa mwamuzi wa ligi ya Oberliga ya wanaume mnamo1998 hadi 2003. Mnamo 2007 Fornaçon alistaafu kazi ya uamuzi. Kwa sasa anaendesha shughuli zake kama mwangalizi wa waamuzi wengine na yuko kwenye kamati ya waamuzi ya Niedersächsischer Fußballverband ( Chama cha Soka huko Lower-Saxony).
Marejeo
hariri- ↑ Women's World Cup Team Game Capsules Archived 2006-05-13 at the Wayback Machine
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Monika Fornaçon kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |