Morenita
Morenita ni jina la kutaja albamu ya kundi zima la muziki wa dansi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo maarufu kama Soukous Stars. Albamu imetoka mwaka wa 1993. Sehemu kubwa ya utayarishaji wa albamu hii ulifanyika nchini Ufaransa katika studio za Galaxy Sound Studios na Studio Harry Son.
Morenita | ||
---|---|---|
Studio album ya Soukous Stars | ||
Imetolewa | 1993 | |
Aina | Soukous | |
Urefu | 37.46 | |
Lebo | Galaxy Sound Studios na Studio Harry Son | |
Mtayarishaji | Soukous Stars |
Orodha ya nyimbo
haririOrodha ya nyimbo pamoja na watunzi wake. Katika muziki wa Afrika, mara nyingi njia ya usambazaji wa muziki ilikuwa kanda au tepu hivyo jambo la upande A na B ni la kawaida sana.
Upande | Jina la wimbo | Mtunzi | Dakika |
---|---|---|---|
A1 | Robin Pretty | Lucien Bokilo | 5:24 |
A2 | Sophia | Lokassa Yambongo | 5:41 |
A3 | Morenita | Ballou Canta | 5:15 |
A4 | Rhoda | Ngouma Lokito | 5:55 |
B1 | Rosy | Shimita | 5:40 |
B2 | Aba Guimo | Philippe "Saladin" Ferreira | 5:58 |
B3 | Cayina | Yondo Sister | 5:13 |
Kikosi kazi
hariri- Besi gitaa – Ngouma Lokito
- Dramsi – Ti Jean
- Mtayarishaji Mkuu – Emma Helou, Mustapha Sesay
- Vinanda - Abdul Mbacki
- Vinanda, Filimbi, Saxofonie – Andy Suzuki
- Gitaa Kiongozi – Saladin*
- Mtayarishaji - Soukous Stars
- Mpiga Rizimu Gitaa – Lokassa ya mbongo*
- Sauti - waimbaji – Ballou Canta, Lucien Bokilo, Shimita, Yondo Sister
Viungo vya Nje
hariri- Morenita katika wavuti ya Discogs