Yondo Sister
Yondo Kusala Denise (amezaliwa tar. 23 Aprili 1958) ambaye anajulikana zaidi kwa jina la kisanii kama Yondo Sister, ni msanii wa Kikongo. Wengi humwita "malkia wa soukous", "Tina Turner" wa muziki wa dansi barani Afrika. Yondo Sister amepata kuwa mwimbaji mkuu katika bendi ya Soukous Stars kwa miaka kadhaa kabla ya kwenda kufanyakazi kama msanii wa kujitegemea. Uwezo wake wa kuimba iliibuliwa na Lutu Mabangu wakati huo Yondo akiwa kama mnenguahi wa Tabu Ley katika bendi yake ya Rocherettes. Yondo muziki uko katika damu, mzee wake alikuwa akipiga muziki kwa kujifurahisha tu, humo kukajengeka ujasiri wa kutoogopa hadhira. Na mara kadhaa alishiriki katika dansi, polepole na kuja kuwa mwanamuziki kamili na kutoa albamu ya kwanza mwaka 1991.[1]
Yondo Sister | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Yondo Kusala Denise |
Amezaliwa | Zaire, Kongo ya Kibelgiji sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
Kazi yake | Mwimbaji, mwanamuziki |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 1980–hadi sasa |
Studio | Air B. Mas Production, Melodie, T.J.R. Music |
Diskografia
haririBaadhi ya diskografia ya albamu za Yondo Sister.
Marejeo
hariri- ↑ Mahojiano ya Yondo Sister na UKENTV huko Youtube.