Moses Kyeswa
Moses Kyeswa (alizaliwa 12 Aprili 1958) ni mwanariadha mstaafu wa Uganda ambaye alibobea katika mbio za mita 400.
Kyeswa alimaliza wa saba katika mbio za kupokezana za mita 4 x 400 katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto ya mwaka 1984 pamoja na wachezaji wenzake John Goville, Peter Rwamuhanda na Mike Okot, katika rekodi ya kitaifa ya dakika 3:02.09. [1]
Kwa kiwango cha mtu binafsi, alishiriki katika mbio za mita 400 katika Michezo ya Olimpiki mwaka 1984 bila kufika fainali. Alifika nusu fainali kwenye Mashindano ya Dunia ya 1983. Akiwa nchini Uswidi, alishinda ubingwa wa Uswidi mwaka 1986, 1987 na 1988.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Moses Kyeswa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |