Moses Masika Wetangula (amezaliwa 13 Septemba 1956) ni mwanasiasa wa Kenya na Mbunge anayewakilisha eneo bunge la Sirisia. Yeye amekuwa Waziri wa Mambo ya Nje tangu Januari 2008.

Moses Wetangula, 2024.

Maisha ya utotoni

hariri

Wetangula alisoma katika Shule ya Msingi ya Nalondo, halafu akaenda katika Shule ya Upili ya Teremi na baadaye Shule ya Friends, Kamusinga kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi, ambapo alifuzu kwa shahada ya Sheria (LLB).

Yeye aliteuliwa kuwa mbunge kwenye chema cha kisiasa cha Kanu baada ya uchaguzi mkuu mwaka 1992, na kuwahudumia Wakenya hadi 1997. Yeye amewahi kushika vyeo vingine kadhaa vya umma kama hakimu na mwenyekiti wa Electricity Regulatory Board. Wetangula alishiriki katika asasi kadha za kuleta fedha ili kuanzisha miradi ya kusaidia watu na amekuwa akitoa huduma za kisheria kwa wananchi. Yeye huhamasisha wanawake na vijana kuanzisha miradi ya kuzalisha kipato.

Wetangula alichaguliwa kwenye Bunge katika uchaguzi wa Desemba 2007. Rais Mwai Kibaki alimchagua Wetangula kuwa Waziri wa Mambo ya Nje mnamo [1] tarehe 8 Januari 2008, pindi kulipokuwa na migogoro kuhusu matokeo ya uchaguzi wa rais. Mwezi wa Januari, baada ya nchi ya Uingereza kulalamika kuhusu uchaguzi wa rais, Wetangula alimwita na kumlalamikia Kamishna wa Uingereza , Adam Wood, na alisema kwamba "uchaguzi wetu hauhitaji muhuri wa mamlaka kutoka House of Commons ".[2] Baada ya serikali ya mseto kukubaliwa kati ya Kibaki na Raila Odinga, wote ambao walidai ushindi katika uchaguzi wa rais, Wetangula bado alihifadhi cheo chake katika Serikali ya Mseto, iliyotangazwa tarehe 13 Aprili 2008.[3]

Marejeo

hariri
  1. "Kenya: Kibaki achagua bara", The East African Standard (allAfrica.com), 8 Januari 2008.
  2. "Kenya kususia upinzani katika mpango wa", Al Jazeera, 21 Januari 2008.
  3. Anthony Kariuki, " Kibaki amtaja Raila PM katika baraza jipya", nationmedia.com, 13 Aprili 2008.

Viungo vya nje

hariri