Netiboli

(Elekezwa kutoka Mpira wa pete)

Netiboli (kutoka Kiingereza "netball"; pia "mpira wa pete") ni mchezo unaotumia mpira ambao huchezwa sana na wanawake.

Mchezo wa Netiboli

Waanzilishi wa mchezo huo walikuwa Waingereza mnamo mwaka 1890.

Kawaida ya mchezo huo ni kwamba huchezwa na timu mbili na kila timu inakuwa na wachezaji saba.

Kutoka katika kila upande wa wachezaji 7, wachezaji hao hujulikana kama GK (Goal Keeper), GS (Goal Shooter), WD (Wing Defense), GD (Goal Defense), WA (Wing Attack), GA (Goal Attack), C (Center): hizo ndizo nafasi za wachezaji.

Sheria za mchezo

hariri

1. Mchezaji haruhusiwi kupiga tambo zaidi ya mbili mara baada ya kupokea mpira (kushika).

2. Mchezaji haruhusiwi kudundisha mpira mara mbili pindi akamatapo mpira.

3. Mchezaji hutakiwa kukaa na mpira ndani ya sekunde 3 tu, hivyo akizidisha mpira huchukuliwa na kupewa timu pinzani kama pasi ya bure (free pass).

  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Netiboli kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.