Mshelisheli
(Artocarpus altilis)
Mshelisheli
Mshelisheli
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Rosales (Mimea kama mwaridi)
Familia: Moraceae (Mimea iliyo na mnasaba na mforosadi)
Jenasi: Artocarpus
Spishi: A. altilis
(Parkinson) Fosberg

Mshelisheli (Artocarpus altilis) ni mti wa familia Moraceae. Matunda yake huitwa mashelisheli. Asili ya mti huu ni Nyugini. Wapolinesi wamepanda mshelisheli visiwani kwa Bahari ya Pasifiki isipokuwa Nyuzilandi na Kisiwa cha Pasaka ambapo hali ya hewa ni baridi sana. Sikuhizi hupandwa mahali pengi pa kanda ya tropiki ambapo kunanyesha kiasi (zaidi ya mm 1500 kwa mwaka).

Picha hariri

  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mshelisheli kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.