Msinduzi
Msinduzi | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Msinduzi (Croton talaeporos) ni mti wa nusufamilia Crotonoideae katika familia Euphorbiaceae. Unatokea pwani ya Kenya na Somalia ya Kusini katika misitu wazi na nyika yenye miti au vichaka.
Spishi hii ni kichaka au mti mdogo wa urefu wa m 2-10. Gome lake ni kijivu na lina nyufa. Majani yana umbo la yai pana, msingi mviringo au wa umbo la moyo, ncha kali au butu, ukingo wenye meno ya mviringo, sm 4-16 kwa 3-15, yenye nywele chache lakini baadaye bila nywele. Maua ni meupe au njano iliyofifia yenye urefu wa mm 2-3, yenye jinsia moja au mbili, katika vishada vya urefu wa sm 8-20 (yote ya kiume au ya jinsia zilizochanganywa). Matunda mekundu au kahawia, karibu umbo la donge au ndewe tatu, mm 20-28 kwa 22-25 mm, yenye nywele.
Matumizi
haririMizizi hutumika kama dawa ya mafua na ya malalamiko ya tumbo.
Marejeo
hariri- ↑ Beentje, H.J. (1994) Kenya trees, shrubs and lianas. National Museums of Kenya, Nairobi.