Mstafeli
Mstafeli (Annona muricata) | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mstafeli
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
|
Mstafeli ni mti mdogo wa familia Annonaceae. Matunda yake yanayolika huitwa mastafeli. Mti huu una maua madogo ya rangi ya njanokijani yenye petali nene. Matunda yana umbo wa yai au figo na rangi ya majani na yana miiba myororo. Nyama ni nyeupe yenye ladha tamu na chachu. Mbegu zake ni nyeusi na kubwa kiasi.
Picha
hariri-
Ua
-
Stafeli
-
Stafeli lililokatwa