Mtango
Mtango (Cucumis sativus) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Mtango shambani
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Mtango (Cucumis sativus) ni mmea mtambaa wa familia Cucurbitaceae. Matunda yake, yaitwayo matango, hutumika sana katika saladi duniani kote.
Spishi mbili za pori huitwa mtango-mwitu (Cucumis aculeatus na C. dipsaceus). Lakini mtango-tamu (Solanum muricatum) hauna mnasaba na mtango, kwa sababu ni mwana wa familia Solanaceae.