Mto Bushman
Mto Bushman (kwa Kiafrikaans: Boesmansrivier) ni mkondo unaotoa maji katika mashariki kwenda kaskazini mashariki mwa mto Tugela, ndani ya KwaZulu-Natal, jimbo la Afrika Kusini.
Mto huo unatoka milima ya Drakensberg, huku eneo lake la juu la kukusanya maji likiwa katika Giant's Castle Game Reserve, mashariki mwa Giant's Castle. Mto huu hupeleka maji yake katika Wagendrift Dam na huendelea kutiririka na kupita katika mji wa Estcourt na hapo huungana na mto Tugela karibu na mji wa Weenen.[1]
Matawimto ya mto huu ni Little Bushmans River ambao huungana na mto Bushman katika Estcourt, Rensburgspruit, mto Mtontwanes na mto Mugwenya. Lambo la Wagendrift karibu na Estcourt ni bwawa kubwa la kuhifadhia maji. Kuna vijiji vingi vyenye idadi kubwa ya watu, vingi vikiwa vinakaliwa na jamii ya amaHlubi, vinapatikana katika eneo la juu la kukusanyia maji.[2] Mto umepakana na Bloukrans River upande wa kaskazini na Mooi River upande wa kusini.
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ "Rivers in South Africa - e-wise". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-22. Iliwekwa mnamo 2009-12-31.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help) - ↑ Pearce, R.O. (1973). Barrier of Spears - Drama of the Drakensberg. Howard Timins. ku. 3–13. ISBN 0 86978 050 6.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Bushman kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |