Mto Nairobi
Mto Nairobi ni mto unaopitia Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Ndio mto mkuu katika beseni la mito ya Nairobi, mtandao wa mito kadhaa inayopita sambamba kuelekea mashariki. Mito yote katika beseni hilo hukutana mashariki mwa Nairobi na kuungana na Mto Athi, hatimaye kuelekea Bahari ya Hindi.
Mingi kati ya mito hii ni myembamba na michafu sana. Mito ya Nairobi huchafuliwa na taka kutoka kilimo, makazi duni na viwanda[1].
Mkondo mkuu, Mto Nairobi, umeweka mpaka wa kaskazini mwa jiji. Mto huu umefanywa kanali katika sehemu nyingine.
Mto Nairobi una vijito kadhaa, kama vile (katika utaratibu wa kushuka kutoka kaskazini hadi kusini):
- Mto Ruiru
- Mto Kamiti
- Mto Rui Ruaka
- Mto Karura
- Mto Gitathuru (ama Getathuru)
- Mto Mathare
- Mto Nairobi (kanali kuu)
- Mto Kirichwa
- Mto Motoine-Ngong
Mto Motoine unafululiza katika Dimbwi la Nairobi, ziwa lililofanywa na wanadamu kutoa maji ya kunywa kwa wakazi wa Nairobi. Mbele zaidi huendelea kama Mto Ngong.
Baadhi ya kingo za mito pia zinajulikana kwa sifa mbaya ya ukosefu wa usalama. Mito hii hugawanya mji kutokana na ukosefu wa mapito yafaayo.
Wakati wa misimu ya mvua maji huongezeka, na kusababisha athari ya mafuriko katika mito yenye kingo zilizo chini.
Tazama pia
haririRamani
hariri- [1] Ilihifadhiwa 11 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
Marejeo
hariri- ↑ Biosafety News, Oktoba / Novemba 2002: Uchafuzi wa Mto Nairobi tisho kwa afya Ilihifadhiwa 23 Oktoba 2006 kwenye Wayback Machine.
Viungo vya nje
hariri- UNEP: Mpango wa Beseni ya Mito ya Nairobi Ilihifadhiwa 9 Oktoba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Geonames.org
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Nairobi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |