Mtukutiko wa homa (pia unajulikana kama mikazo ya homa au msukosuko wa homa) ni mtukutiko wa homa unaohusiana na halijoto ya mwili lakini bila hatari yoyote kwa afya. Hutokea mara nyingi kwa watoto kati ya umri wa miezi sita na miaka 5.[1] Mitukutiko mingi huwa chini ya dakika tano kwa wakati mmoja na mtoto anarudi katika hali yake ya kawaida kabisa chini ya dakika sitini ya tukio.[1][2]

Mtukutiko wa homa
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuNeurology, emergency medicine, pediatrics Edit this on Wikidata
ICD-10R56.0
ICD-9780.31
OMIM604352
DiseasesDB4777
MedlinePlus000980
eMedicineneuro/134
MeSHD003294

Kisababishi na utambuzi

hariri

Mitukutiko ya homa inaweza kuwa kwa familia. Utambuzi inahusisha uidhinishaji kuwa hakuna maambukizi kwa ubongo, na hakuna matatizo ya metaboli, na hayajakuwa kabla ya kutokea kwa mitukutiko iliyotokea bila homa. Kuna aina mbili za mitukutiko ya homa, kuna mtukutiko wa homa rahisi na mtukutiko wa homa ulio ngumu. Mtukutiko wa homa rahisi unahusisha mtoto aliye na afya ambaye amekuwa na toni ya mtukutiko wa kloni inayodumu chini ya dakika 15 kwa muda wa masaa 24. Uchunguzi wa damu, na kupiga picha ubongo au ensefalogramu (MUU) hauhitajiki kwa utambuzi. Uchunguzi wa kubaini chanzo cha homa unapendekezwa. Kwa watoto wengine wanaoonekana kuwa na afya pancha ya kiuno haihitajiki.[1]

Uzuiaji, udhibiti, prognosi na epidemolojia

hariri

Dawa ya kuzuia mtukutiko au dawa ya homa haipendekezwi kwa juhudi za kuzuia mitukutiko rahisi ya homa zaidi.[1] Kwa hali chache zinazodumu zaidi ya dakika tano benzodiazepini kama vile lorazepamu au Midazolam inaweza kutumika.[1][3] Matokeo kwa kawaida huwa bora na matokeo sawa ya mtihani kwa watoto wengine na hakuna mabadiliko kwa hatari ya kifo kwa wale walio na mitukutiko rahisi ya homa. Kuna ushahidi wa muda mfupi kuwa watoto wako na ongezeko kiasi la hatari ya kifafa kwa asilimia 2.[1] Mitukutiko ya homa huathiri asilimia mbili hadi kumi ya watoto kabla ya umri wa miaka mitano.[1][4] Huwa ni nyingi kwa wavulana kuliko wasichana.[5] Baada ya mtukutiko mmoja wa homa kuna uwezekano wa asilimia 15 hadi 70 ya kuwepo kwa nyingine.[1]

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Febrile seizures: risks, evaluation, and prognosis". American family physician. 85 (2): 149–53. Jan 15, 2012. PMID 22335215. {{cite journal}}: Cite uses deprecated parameter |authors= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Symptoms of febrile seizures". www.nhs.uk. 01/10/2012. Iliwekwa mnamo 13 October 2014. {{cite web}}: Check date values in: |date= (help)
  3. Paritosh Prasad (2013). Pocket Pediatrics: The Massachusetts General Hospital for Children Handbook of Pediatrics. Lippincott Williams & Wilkins. uk. 419. ISBN 9781469830094.
  4. Patterson, JL; Carapetian, SA; Hageman, JR; Kelley, KR (Des 2013). "Febrile seizures". Pediatric annals. 42 (12): 249–54. doi:10.3928/00904481-20131122-09. PMID 24295158.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Ronald M. Perkin, mhr. (2008). Pediatric hospital medicine : textbook of inpatient management (tol. la 2nd ed.). Philadelphia: Wolters Kluwer Health/Lippincott Williams & Wilkins. uk. 266. ISBN 9780781770323. {{cite book}}: |edition= has extra text (help)
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtukutiko wa homa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.