Mtumiaji:Kipala/Archive 4
Fragen zur sw.Wikipedia
Hallo, ich würde mich freuen, wenn du mich per E-mail kontaktieren würdest. Ich mache eine kleine Studie zu verschiedenen Wikipedias. pzvanpdwijk@wgooglemail.com (bitte entferne die Buchstaben, mit denen Paula und Willibald anfangen).
Jamii
Kipala, shikamoo! Pole kwa kuchelewa kukujibu. Ni sawa usemavyo. Kila jamii inatakiwa iwe hivyo usemavyo, kwani inakuwa tayari ishaundwa. Vinginevyo itabaki kuwa nyekundu ilhali kuna zingine zitakuja. Lakini bado nina swali moja: Sina uhakika kama hapa katika Wikipedia hii twaita Ukraine? Au kuna jina lingine tofauti (maandishi namna yanavyoandikwa juu ya Ukraine - Yukreini?) Ndiyo sababu iliyopelekea mimi kutoanzisha jamii zile. Hapo vipi.--Mwanaharakati (majadiliano) 05:07, 2 Mei 2008 (UTC)
- Asante kwa swali. Katika makala mbalimbali nimetumia "Ukraine". Yukreini sijaona bado. Wala sijaiona kwenye google. "Yukreini" ni matamshi ya Kiingereza kwa maandishi ya Kiswahili. Ila tu Waingereza/Wamarekani kwa jumla hutamka nchi nying kwa namna yao (Tenzenia; Tenzeenya). Nimeona mtindo huu unaofuata matamshi ya Kiingereza kwa nchi mbalimbali katika orodha za Radio Tanzania au hata TUKI. Ila tu kama sijaona ni kawaida kweli sijaitumia hapa. -- Nchi ile tunayojadili wanajiita wenye "Ukrayina"; kimataifa mara nyingi huandikwa "Ukraine" na kila mmoja anaitamka kufuatana na lugha yake. Je, unaona tatizo? --Kipala (majadiliano) 06:59, 3 Mei 2008 (UTC)
- Naona Kamusi Hai wana "Ukraini" --Kipala (majadiliano) 07:06, 3 Mei 2008 (UTC)
- Asante kwa swali. Katika makala mbalimbali nimetumia "Ukraine". Yukreini sijaona bado. Wala sijaiona kwenye google. "Yukreini" ni matamshi ya Kiingereza kwa maandishi ya Kiswahili. Ila tu Waingereza/Wamarekani kwa jumla hutamka nchi nying kwa namna yao (Tenzenia; Tenzeenya). Nimeona mtindo huu unaofuata matamshi ya Kiingereza kwa nchi mbalimbali katika orodha za Radio Tanzania au hata TUKI. Ila tu kama sijaona ni kawaida kweli sijaitumia hapa. -- Nchi ile tunayojadili wanajiita wenye "Ukrayina"; kimataifa mara nyingi huandikwa "Ukraine" na kila mmoja anaitamka kufuatana na lugha yake. Je, unaona tatizo? --Kipala (majadiliano) 06:59, 3 Mei 2008 (UTC)
Sawa. Lakini bado hatuna sababu za kubadilisha kwakuwa itatugharimu sehemu kubwa ya Wikipedia yetu. Ni bora tuweke tu hiyo hiyo "Ukraine". Ahksante kwa taarifa yako! Kazi njema...--Mwanaharakati (majadiliano) 13:35, 3 Mei 2008 (UTC)
Takl:Fransisko
Salam. Samahani mkubwa. Mbona umehondosha haya:
Ricardo amerudisha umbo la makala "Fransisko wa Asizi" jinsi ilivyokuwa awali. Umbo hili si kawaida katika wikipedia na hasa haifai kwa makala ndefu. Maana yake jinsi alivyoandika inazuia kutokea kwa orodha ya yaliyomo. Orodha hii inatakiwa ni msaada. Naomba atafakari haya. Akiona sababu ya kuacha umbo jinsi ilivyo tafadhali atueleze. Nitasubiri nisiposikia kitu nitarudisha mabadiliko niliyoingiza awali.
Kumbukumbu ya uhondoshaji ni: http://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Talk:Fransisko_wa_Asizi&oldid=132177.
Samahani lakini...--Mwanaharakati (majadiliano) 13:52, 14 Mei 2008 (UTC)
- Labda ilikuwa kosa kuliondoa lakini nilikosa kuandika kwa sababu yeye alirudisha badiliko yeye mwenyewe; sijaendelea kusoma. Sijui nirudishe na kuongeza elezo? --Kipala (majadiliano) 14:02, 14 Mei 2008 (UTC)
- Itakuwa vyema zaidi ukifanya hivyo.--Mwanaharakati (majadiliano) 14:48, 14 Mei 2008 (UTC)
Ndugu Kipala, samahani kama nimewakwaza kugusagusa tena makala ya Fransisko. Sikudharau mchango wako wa kupenda yaliyomo yaonekane, ila namba zilikuwa zinaonekana dabodabo. Baada ya kujaribu mara mbili tatu nimefaulu kufanya ziwe sawa. Pia nafasi yangu katika mtandao ni ndogo na pengine nashindwa kuwasiliana nanyi mlio wazoefu zaidi. Usisahau kubadilisha "Klara" kuwa "Klara wa Asizi" kama ulivyobadilisha "Ualimu" kuwa "Ualimu wa Kanisa". Salamu kwa Mwanaharakati anayestahili zaidi kupongezwa kwa kufikia makala 7,000. Tulenge 10,000 na kupiku lugha ya Afrikaans!
A little help: Ecser
Salam! Hi! I'm a Hungarian Wikipedia editor, my name is Norbert Kiss. I'm very proud of my village and I would like to read about it in a lot of langauges. I translated already it into 10 languages, but I can't speak KiSwahili. Could you help me. My village's English page is this: Ecser. Could you translate the page of Ecser into KiSwahili? Then just link the side into the English version and I will see it, or you could write me, when it is ready. My hungarian Wikipedia side is: My profile. Or my e-mail is: eino@freemail.hu
Thank you! Norbert
- Dear Norbert, I appreciate your endeavour but I think we should not do it. In a small wikipedia like ours there is lots of other things to do and frankly we could get a "relevance" - debate. Please do come back once we are over 20,000 entries. --Kipala (majadiliano) 09:34, 18 Mei 2008 (UTC)
- Ahksante kwa masahihisho yako! Naona umeanzisha makala mpya ya "Utawala huria". Huwa najaribu-jaribu kuandika habari za wanaharakati kama hao, lakini mara nyingi juhudi zangu zinagonga mwamba kwa ufinyu wa lugha, najikuta natafsiri neno kinamna vingine. Labda niahidiwe masawazisho pindi niandikapo makala za namna hiyo kisha kuwe na mtu wa kuzisawazisha. Muziki na filamu, oooh, mashallah nazimanya! Ni hayo tu. Wako katika ujenzi wa Wikii hii,--Mwanaharakati (majadiliano) 08:40, 16 Mei 2008 (UTC)
- Haya tuendelee kusaidiana! --Kipala (majadiliano) 21:56, 16 Mei 2008 (UTC)
Botflag
Baada ya kuingia chini ya jina lako (kwa vile wewe ni bureaucrat - asiye bureaucrat haruhusiwi), uendee ukurasa wa http://sw.wikipedia.org/wiki/Special:Makebot, utaingiza jina la mtumiaji ambaye ungehitaji kumfanyia akaunti ya kikaragosi, na mambo yafuatayo yatajieleza. Wasalaam! --Baba Tabita (majadiliano) 14:24, 19 Mei 2008 (UTC)
TUSC token b5b8d92cdae975430ce1b1b3375e38a2
I am now proud owner of a TUSC account!
Salam! Samahani mzee wangu. Naomba nitafsirie maana nzima ya kichwa cha habari husika hapo juu.
- National Front for the Liberation of South Vietnam.
Tafwadhali!--Mwanaharakati (majadiliano) 13:11, 20 Mei 2008 (UTC)
- Umoja wa Kizalendo kwa Ukombozi wa Vietnam Kusini; labda heri uweke kiungo cha Vietkong kwa sababu hii ilikuwa jina lao la kawaida kimataifa jinsi ninavyokumbuka na nitaandia makala. --Kipala (majadiliano) 15:32, 20 Mei 2008 (UTC)
- Dah! Utakuwa umefanya la maana sana kama utaiandikia makala. Nilikuwa na mpango wa kuiandika, mizali umesema utaiandikia itakuwa bora zaidi kwanini wewe utailezea vyema! Nasubiria matokeo.....--Mwanaharakati (majadiliano) 15:51, 20 Mei 2008 (UTC)
Salam. Samahani kidogo. Unaonaje ukifanya masahihisho kidogo katika makala ya "Mauaji ya Halaiki ya My Lai", kwasababu katika makala hiyo inataja sehemu kadhaa ya Vietkong. Nitashukuru kama utafanya hivyo.--Mwanaharakati (majadiliano) 05:37, 21 Mei 2008 (UTC)
- Haya, nimeongeza kidogo. --Kipala (majadiliano) 10:54, 21 Mei 2008 (UTC)
Imekuwa imara kabisa. Ahksante kwa kuitikia!--Mwanaharakati (majadiliano) 12:38, 21 Mei 2008 (UTC)
Kipala, salam. Kuna kitu nataka kujua kiundani hasa. Kitu chenyewe ni "Vampire". Hawa mavempaya walikuwepo kweli au ni hadithi tu za hapa na pale? Labda ingekuwa poa zaidi kama utaandika makala ya Vampire katika wiki yetu! Pia nitashukuru zaidi kama utaanza kunijibu kabla ya kuandika! Ubarikiwe,--Mwanaharakati (majadiliano) 11:24, 22 Mei 2008 (UTC)
- Somo hili - Bwana sijui. Kwa makala yenye maana nahitaji kusoma kwa sabbu sijui habari zinalangana na imani zipi za Afrika Mashariki. -- Kuna mambo mengi yanayangiana: imani ya kuwepo kwa watu wanaonyonya damu (vampir ni pia aina ya popo ya Asia inayonya damu kweli), imani ya kuwepo kwa watu wasiokufa kamili lakini wanalala makaburini tu na wakati mwingine wanatoka makaburini kumbe ni kama imani kuhusu wachawi katika pande nyingi za dunia. Hakuna dalili ya kwamba wako au walikuwepo lakini imani iko mahali mbalimbali na kuleta hofu. Tangu kupatikana kwa filamu kila mtoto kwetu ameona habari zao. --Kipala (majadiliano) 16:55, 22 Mei 2008 (UTC)
Bot
Salam nyingi, Kipala. Naomba kuuliza kidooogo. Hapa naona mara kwa mara maelezo ya mtumiaji mpya yakiambatana na maneno (Account created automatcally), hiyo ndiyo nini? a)(b Bot hutengenezwa na mtumiaji au Mrasimu? Kwani hata ukifungua kurasa ya mtumiaji anayeonekana kuwa yeye ni bot, basi huomba msaada kutoka kwa Mrasimu ili aweze kupata haki za bot! Sasa sijui hapo inakuwaje?--Mwanaharakati (majadiliano) 07:10, 28 Mei 2008 (UTC)
- Salaam Muddy, asante kwa swali lakini sijui kujibu namna gani. Hata mimi nilishangaa juu ya akaunti nyingi zilizojitokeza mara moja. Labda kuna utaratibu mpya kwenye wikipedia ngazi ya juu ya kwamba Bot inaweza kuomba kibali cha bot kwa wikipedia mbalimbali mara moja na anapewa. Nimemwuliza mmoja wa watu wale kwenye ukurasa wake kwenye de:wiki kama anajua imekuwaje. --Kipala (majadiliano) 10:17, 28 Mei 2008 (UTC)
- Sawa. Mimi naweza kuwa Bot? Ukiangalia marejeo ya ukurasa wa Jumuiya unasema: Mrasimu (Bureaucrat) (ni neno la Kiingereza, maana ni mfanyakazi wa uendeshaji wa serikali au ushirika mwingine) ana uwezo kufanya mtu kuwa mkabidhi, kubadilisha jina la mtumiaji na kuteua akaunti ya kikaragosi ("set bot flag", kwa kiingereza). Kwanini swali liwepo? (Inaonekana Bot inaumbwa na wewe mwenywe na si-vinginevyo). Sharti uwe Mrasimu tu. Vipi nauliza na kufuatilia haya? Ni mda sasa huwa na fikiria na kuuliza swali juu ya haya Mabot, lakini hamna anayejibu juu ya hili. Mimi binafsi nimefikiria na nikaona kwamba, upo uwezekano wa haya Mambot kuumbwa na Mrasimu, yaani kama unavyosema ukurasa wa Jumuiya kuhusu Mrasimu. Sijui wewe mwenzangu unafikiriaje juu ya hilo?--Mwanaharakati (majadiliano) 11:53, 28 Mei 2008 (UTC)
- Bot ni programu iliyoandikwa na mtumiaji au programu inayotumiwa na mtumiaji inayorekebisha au kuongeza sehemu za makala. Mfano ni kuingiza interwiki. Hapa programu inaambiwa kupita kwenye wikipedia zote na kutazama kama kicha cha makala fulani iko katika wiki hizi. Kama haiko programu inaandika. Au kile nilichofanya jana kwa mkono yaani moja-moja: nilikumbushwa na sahihisho la Ndesanjo ya kwamba si "Jamhuri ya maungo ya TZ" lakini "muungano wa". Basi nikapita na kusahihisha. Kama ningejua ningeandika programu ya bt na hii ingefanya. -- Basi ukijua haya andika. Menginevyo: hapana. Mimi sijui kuandika programuy a Bot.-- Utaratibu wa kuikubali bot ni ya kwamba programu baya inaweza kuleta hasara na fujo kwa hiyo wanatakiwa kuomba kibali cha wasimamizi baada ya majaribio ya kwanza. Lakini mara nyingi wanapuuza na mimi sijafuatilia siasa juuy a bot ni ipi sasa. Nikiona Bot imerudia mara kwa mara bila hasara nimeamua kuipa bendera ya Bot na faida yake ni haionekani tena katika orodha ya mabadiliko nisipotaka na hii inasaidia kuona mabadiliko yenye maana. --Kipala (majadiliano) 12:05, 28 Mei 2008 (UTC)
- Sawa. Mimi naweza kuwa Bot? Ukiangalia marejeo ya ukurasa wa Jumuiya unasema: Mrasimu (Bureaucrat) (ni neno la Kiingereza, maana ni mfanyakazi wa uendeshaji wa serikali au ushirika mwingine) ana uwezo kufanya mtu kuwa mkabidhi, kubadilisha jina la mtumiaji na kuteua akaunti ya kikaragosi ("set bot flag", kwa kiingereza). Kwanini swali liwepo? (Inaonekana Bot inaumbwa na wewe mwenywe na si-vinginevyo). Sharti uwe Mrasimu tu. Vipi nauliza na kufuatilia haya? Ni mda sasa huwa na fikiria na kuuliza swali juu ya haya Mabot, lakini hamna anayejibu juu ya hili. Mimi binafsi nimefikiria na nikaona kwamba, upo uwezekano wa haya Mambot kuumbwa na Mrasimu, yaani kama unavyosema ukurasa wa Jumuiya kuhusu Mrasimu. Sijui wewe mwenzangu unafikiriaje juu ya hilo?--Mwanaharakati (majadiliano) 11:53, 28 Mei 2008 (UTC)
Samahani kwa kukushughulisha mzee wangu. Pia napenda kukushukuru kwa majibu yako yaliyojawa na busara tele. Basi ni hayo tu niliokuwa nayo na baada ya hapo ni kusema tu kazi njema! Nipo najaribu kuandika mambo ya mpira wa miguu. Hata hivyo sina uzoefu wowote kuhusu mpira wa miguu, lakini najaribu kuandika hizi habari kwakuwa katika Wikipedia yetu habari hizo ni hafifu mno. Hivyo najaribu kuziorodhesha kwani hata watu wakija wapate kuona kumbe hata habari za mpira pia zipo!!!--Mwanaharakati (majadiliano) 12:45, 28 Mei 2008 (UTC)
- Nimepata jibu - kuna utaratibu mpya ya kwamba mtumiaji wa wikipedia yoyote anayeanzisha "global account" (hii sina uhakika ni nini) anafunguliwa akaunti katika kila wikipedia anapoingia kwa kutaipi jina lake.--Kipala (majadiliano) 06:46, 29 Mei 2008 (UTC)
- Namimi ninayo global account. Unafanya hivi: http://sw.wikipedia.org/wiki/Special:MergeAccount hapo ukikubali tu kufanya hivyo, ujue kila sehemu utakapoingia unakuwa huna haja ya kuanzisha akaunti nyingine. Lakini nilisahau kama nilishawahi kufanya hicho kitu. Yenyewe inasaidia kama atatokea mtu mwingine akataka kujisajiri kwa jina sawa na lile la kwako ile inakataa kumsajili huyo mtu. Hata hivyo shukurani za dhati zikufikie kwa kazi yako ulioifanya juu ya uchambuzi wa habari kuhusu accout created automatically! Ubarikiwe!--Mwanaharakati (majadiliano) 08:16, 29 Mei 2008 (UTC)
Biblia
Ndugu, asante kwa maelekezo yako. Bila ya shaka napenda kushirikiana, ila sikujua mengi kati ya hayo uliyoniandikia. Nitakuwa macho zaidi, lakini mambo ya kujifunza ni mengi. Nikikosea, msahihishe nyinyi mliozoea zaidi. Kosa moja nililolitambua lakini sijui kusahihisha ni kwamba makala moja niliyoandika ina kichwa "Barua ya Kwanza kwa Watesalonike" badala ya "... Wathesalonike". Naomba urekebishe. Ile njia ya ku-redirect sijaielewa. Asante. Salaam!
Ndugu, pole kwa kazi nyingi unazoifanyia Wiki. Nasubiri bado uingize Deuterokanoni 7 katika lebo ya Agano la Kale. Pia nimeingiza ile ya Agano Jipya katika vitabu vyote vilivyokuwa havina, lakini kuna shida: imeandikwa Galata na Thesaloniki, tofauti na kurasa husika. Naomba uirekebishe mambo yawe sawa. Mimi siwezi. Hatimaye naomba tena uangalie usilinganishe "Biblia ya Kiebrania" na "Agano la Kale" kama ni kitu kimoja: kwa Wakristo walio wengi sivyo, kwa kuwa Agano la Kale lina vitabu 7 na sehemu nyingine ambazo hazimo katika Tanakh. Wasalamu --Riccardo Riccioni (majadiliano) 21:40, 16 Julai 2008 (UTC)
Namaanisha zile lebo zilizopangwa chini ya ukurasa "Agano la Kale" na ya vitabu vyake mbalimbali, zenye majina ya vitabu vyote yakiwa na viungo husika. Katika vitabu vya "Agano Jipya" viko pembeni.
- Nimeelewa. Ilikuwa Template:Biblia_AK. Nimesahihisha. Halafu ilikuwa nini juu ya kulinganisha "Biblia ya Kiebrania" na "Agano la Kale"? --Kipala (majadiliano) 07:41, 17 Julai 2008 (UTC)
Hi Kipala! :)
Dear Kipala,
Hi! Could you please help me create a short translation-stub of this article in German for the Kiswahili Wiki? Any help would be greatly appreciated as it may serve for development in the future. All my best, Girl from the Village (majadiliano) 09:55, 3 Juni 2008 (UTC)
- Iko tayari. Angalia: Chama cha Uhuru cha Puerto Rico. --Kipala (majadiliano) 11:36, 3 Juni 2008 (UTC)
Mdau
Salam. Kusema kweli sijui maanake halisi. Lakini nitajaribu kuelezea vile ninavyoona mimi. Mdau mara nyingi inakuwa viongozi au watu wenye kupaumbele katika jambo fulani au hata ukisema wakeletwa au wanachama-mwanachama wa damu ndiyo mdau. Hivyo akiona jambo lolote linaenda kinyume na taratibu za chama au timu ya mpira wadau wa chama au wadau wa timu huanza kulalama juu ya jambo au uamuzi kichama. Hata mimi ni mdau wa Wikipedia natumai nawe ni mmoja wao! Ama sivyo?--Mwanaharakati (majadiliano) 15:01, 4 Juni 2008 (UTC)
- Nimeona tena. Uliandika "Dau". Dau sijui ndiyo boti (sail bot). Hivyo washika dau inakuja kutokana na neno hilo Dau, wao wanalishika lisije likazama. Kwa maana nyingine yaani kimtaani: Dau, maanake fedha, yaani hela pia uitwa dau, lakini kimtaa mtaa. Hapo vipi.--Mwanaharakati (majadiliano) 15:18, 4 Juni 2008 (UTC)
- Nasikitika kukueleza kwamba sinto patikana kama awali. Hapa kazini tumepatwa na tatizo la seva. Seva imekorofisha, hivyo tunasubiria hadi hapo itakapokuwa sawa! Hata leo nipo InternetCafe nikiwa nafanya masahihisho kadhaa na kubadili home page. Lakini naamini itakuwa sawa hivi karibuni! Poleni sana Wazungu wangu, kila lakheri!--Mwanaharakati (majadiliano) 15:14, 7 Juni 2008 (UTC)
- Pole sana nategemea utarudi! --Kipala (majadiliano) 15:32, 8 Juni 2008 (UTC)
- Nasikitika kukueleza kwamba sinto patikana kama awali. Hapa kazini tumepatwa na tatizo la seva. Seva imekorofisha, hivyo tunasubiria hadi hapo itakapokuwa sawa! Hata leo nipo InternetCafe nikiwa nafanya masahihisho kadhaa na kubadili home page. Lakini naamini itakuwa sawa hivi karibuni! Poleni sana Wazungu wangu, kila lakheri!--Mwanaharakati (majadiliano) 15:14, 7 Juni 2008 (UTC)
- Nimeona tena. Uliandika "Dau". Dau sijui ndiyo boti (sail bot). Hivyo washika dau inakuja kutokana na neno hilo Dau, wao wanalishika lisije likazama. Kwa maana nyingine yaani kimtaani: Dau, maanake fedha, yaani hela pia uitwa dau, lakini kimtaa mtaa. Hapo vipi.--Mwanaharakati (majadiliano) 15:18, 4 Juni 2008 (UTC)
- Dua lako limekubaliwa. Tayari nisharudi kama awali! Basi kila lakheri...--Mwanaharakati (majadiliano) 13:45, 10 Juni 2008 (UTC)
Mtaguso
Ndugu, naomba tena msaada: ufute makala "Concilio Ecumenico": nilikosea lugha ya kichwa, baadaye nikaandika kwa usahihi "Mtaguso Mkuu". Pole kwa usumbufu.
Ndugu, samahani kwa kukusumbua. Nimeelewa mapema sera ya wikipedia na nina nia ya kuifuata. Nikikosea, kuna uwezekano wa kurekebisha. Kila makala si kamili, ni kwa ajili ya kuboreshwa na mtu yeyote. Nitajitahidi kufanya hivyo kwa kutoa habari zaidi za kihistoria. Upande wa lugha ya kimadhehebu, naomba uzingatie kwamba makala juu ya hati za mtaguso zinatakiwa kuelewa ulichosema, hivyo hakuna budi kueleza msimamo wa Wakatoliki uliotamkwa rasmi katika hati hizo: hatuweza kufanya hati hizo zisiseme ziliyoyasema eti, tuwe neutral. Tunaweza kueleza kama watu neutral msimamo wa Kikatoliki uliomo kati hati hizo. Halafu sikulaumu Waprotestanti tu (kuhusu kukanusha ualimu wa Kanisa Katoliki, jambo ambalo liko wazi), bali hata Wakatoliki (kuhusu kutotumia sana Biblia): nadhani hayo ni mambo yasiyopingika. Tena, pengine unabadilisha tofauti na ukweli, kwa mfano kuhusu Christus Dominus, ulivyokuwa umesema askofu katika nafasi ya pili anashughulikia kanisa kitaifa, kumbe ni kijimbo. Vilevile Kanisa la Vatikano si Kanisa kuu, ni Basilika tu: kanisa kuu la Roma ni lile la Mt. Yohane huko Laterano. Mimi ni mwenyeji wa huko. Asante tena kwa bidii zako. Amani kwako. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:28, 22 Juni 2008 (UTC)
- Ndugu Riccardo, asante sana kwa maelezo yako. Naomba tuendelee kuelewana bila samahani. Niseme kwanza ya kwamba hatuwezi kuepukana na tatizo la lugha ya kidhehebu. Tunahitaji kutafuta njia mara kwa mara. Kwa bahati nzuri nilibarikiwa kushirikiana na mapadre wakatoliki kwa miaka kadhaa katika kundi moja la walimu wa dini na hapa nimejifunza kidogo jinsi gani madhehebu yameunda msamiati tofauti juu ya mambo yaleyale; tukianza kujadiliana tunashangaa: Mbona anasema hivi?? Mfano bora ni ya kwamba Wakatoliki huombea "mkate wetu wa kila siku" lakini Walutheri na Waprotestanti wengine "riziki yetu". Na inaendelea.
- Juu ya ualimu wa kanisa - nikitazama haya kwa miwani yangu ya kiluteri sikanushi ualimu wa kanisa katoliki; hata upande wa Kiprotestanti kuna ualimu wa kanisa lakini kuna hoja tofauti juu ya muundo wa kanisa. Kwa hiyo kama "ualimu wa kikatoliki" hainigusu sana - kama mchango katika ualimu wa kanisa la Kristo sawa. Tukiwa na makala hapa hatuna budi kusaidiana ili tupate makala inayoeleweka hata msomaji ni Mwislamu apate kuelewa Wakristo wanamaanisha nini. Vivyo hivyo mengine kuhusu mafundisho. Nadhani kimsingi tuko pamoja ila tu - utekelezaji.
- Kuhusu makala ya mtaguso nilijitahidi tu kuyanyosha kidogo ili yaeleweke vizuri zaidi. Tutaendelea kusahihishana. Nadhani juu ya Christus Dominus ni kweli unachosema. Hata hivyo naona makala imeboreka kwa msomaji nikiangalia jinsi tulivyosahihisha kila mmoja wetu. Nadhani mimi niliweza kuchangia mpangilio wa mwanzo unaosaidia kuelewa vizuri zaidi, na wewe uliondoa kosa kuhusu ngazi ya kitaifa kuwa kijimbo.
- Kuhusu Kanisa Kuu au nini napendekeza mawili.
- Upande moja naona bado unajenga uzoefiu wa wikipedia. Ukiona kiungo cha rangi ya buluu na unaona kasoro ndani yake naomba usibadilishe kiungo hiki kinachonekana nyekundu baadaye. Katika mfano huu: Niliandika tayari makala "Kanisa Kuu la Mt. Petro" na kuweka kiungo katika makala ya Vatikani. Ukibadilisha kiungo tu inabaki kiungo bila lengo (yaani nyekundu) lakini makala yenyewe bado ni vile. Mabadiliko ya aina hii yana maana tu baada ya kusahihisha makala yenyewe.
- kuhusu jina la makala ingekuwa vema kufanya majadiliano huko kwa neno lenyewe. Kwa hiyo ninanakili maoni yako ya juu na kuendelea huko Talk:Kanisa Kuu la Mt. Petro. Wasalaam! --Kipala (majadiliano) 14:03, 22 Juni 2008 (UTC)
Machakos
Hi, könntest du dein Bild http://sw.wikipedia.org/wiki/Image:KE-Machakos.png in Wikimedia Commons reinstellen damit ich das Bild für nen Deutschen Artikel "Machakos" verwenden kann? -- Kenji 19:52, 10. Juni. 2008 (CEST)
Wikikamusi
- Kipala, salam. Unaweza kunisaidia kutafsiri maneno haya kwa Kiswahili?
- das freie worterbucb
- ein-Wiki-basiertes
Maneno yanatoka katika lugha ya Kijerumani, sasa naomba nitafsirie kwa Kiswahili murua kabisa. Kwani hayo maandishi nataka nikaweke katika logo ya Wikamusi kwa Kiswahili! Naona itakuwa bora zaidi Waswahili tukiwa na logo yetu ya Wikamusi. Nitashukuru sana endapo utanisaidia kutafsiri maelezo hayo. Kazi njema...--Mwanaharakati (majadiliano) 16:40, 11 Juni 2008 (UTC)
- Naomba nipe kiungo chake (link) nipate kuona yote. --Kipala (majadiliano) 23:03, 11 Juni 2008 (UTC)
- Angalia hapa: http://de.wiktionary.org/wiki/Wiktionary:Hauptseite
Ni kurasa nzima ya de.wikt. Naomba iangalie ile logo yake kisha unisaidie maana! Nategeme jibu la haraka... Ubarikiwe!--Mwanaharakati (majadiliano) 05:44, 12 Juni 2008 (UTC)
- das freie wörterbuch - KAMUSI YA LUGHA HURU / HURIA
- ein-Wiki-basiertes - KWENYE MSINGI WA WIKI
- wiktionari - WIKIKAMUSI
- Je unataka kuendelea na hii? http://sw.wiktionary.org/wiki/Mwanzo
- --Kipala (majadiliano) 06:04, 12 Juni 2008 (UTC)
- Sijakupata bado. Kuendelea vipi?--Mwanaharakati (majadiliano) 07:09, 12 Juni 2008 (UTC)
- Niliuliza kama unapenda kujenga wikikamusi ile - niliiangalia nikaamua kuiacha kwa sababu msingi ni mdogo mno --Kipala (majadiliano) 14:38, 12 Juni 2008 (UTC)
- Sijakupata bado. Kuendelea vipi?--Mwanaharakati (majadiliano) 07:09, 12 Juni 2008 (UTC)
- Kweli kabisa kule msingi bado mmdogo sana. Ila niko najaribu kuweka baadhi ya vitu vya msingi - kubadilisha maelezo yote ya Kiingereza na kuyaleta kwa Kiswahili na kuboresha baadhi ya kurasa ambazo tayari zimeshaundwa na watu wengine kisha wakazitelekeza. Kama uliona hivi karibuni nimejaribu kuunda template wiktionary kwa lengo la kuelekeza maneno kutoka huku kwenda kule. Na vilevile katika Wiktionary nimetengeneza template wikipedia, ambayo inaonyesha pia baadhi makala za huku. Naona kazi kubwa, lakini nitajitahidi kuimudu. Kule pia nasimama kama mkabidhi wa muda. Ukabidhi wangu utaisha hapo mwezi Novemba na ukisha sinto enda tena kuongezea kwani nitakuwa tayari nimesha umba jumuia kuubwa. Bado najipa imani nitashinda! Wikipedia kwa Kiswahili, ndiyo mwanzilishi wangu na ndiyo mwongozo wangu kwa kila hatua ninayopiga katika Wikamusi. Na ndiyo maana unaniona niko naumba template mpya katika wiki hii. Ila poa tu, tuendelee kubamba...--Mwanaharakati (majadiliano) 16:14, 12 Juni 2008 (UTC)
Salaam! Mkubwa samahani kidogo. Ingawaje nakusumbua mara kwa mara, lakini utafanyaje (Ukubwa Jalala!) Naomba nisaidie maana halisi ya neno "singles chronology". Nikiangalia pale inaonyesha: nyimbo iliyopiata, iliyopo na ijayo. Lakini bado sipati Kiswahili sanifu cha neno "chronology" (sina kamusi hapa kazini). Naomba nisadie!--Mwanaharakati (majadiliano) 06:31, 13 Juni 2008 (UTC)
- Naomba nipe ukurasa unaohusika. --Kipala (majadiliano) 07:08, 13 Juni 2008 (UTC)
- Angalia HAPA...--Mwanaharakati (majadiliano) 07:32, 13 Juni 2008 (UTC)
- Chronology ni wendo au orodha au habari na matukio yaliyopangwa kufuatana na muda/miaka / tarehe. "chronology of events" - ni mpangilio wa matukio katika utaratibu wa wakati; singles chronology ni orodha ya rekodi zake ndogo kufuatana na miaka zilipotolewa. Ningeandika neno kwa "singles" tu na orodha chini yake.--Kipala (majadiliano) 15:38, 13 Juni 2008 (UTC)
- Angalia HAPA...--Mwanaharakati (majadiliano) 07:32, 13 Juni 2008 (UTC)
Ahksante Mzee wangu kwa msaada wako. Nimeweza kufanikisha zoezi hili la "Sanduku la Habari la Single". Ubarikiwe!--Mwanaharakati (majadiliano) 16:41, 13 Juni 2008 (UTC)
Thanks for the bot flag!
I was going to request for it today, but you were faster. --Silvonen (majadiliano) 03:39, 18 Juni 2008 (UTC)
Template
Kipala, salam. Naona kuna balaa tena. Kwangu template zote hazionekani. Na eneo la kuhariri limekaa mkono wa kushoto badala ya kulia. Je hapo kwako vipi?--Mwanaharakati (majadiliano) 06:00, 20 Juni 2008 (UTC)
- Sijaona kitu bado. Naona subiri tu. Kama ni templeti zote ni jini fulani atapotea tena. --Kipala (majadiliano) 06:01, 20 Juni 2008 (UTC)
- Natekeleza ushauri wako. Lakini kwa leo sintowza kuhariri chochote kile.
Kwani hata nikiandika, kuna mpaka wa kuandika! Au ngoja ni-restart mashine yangu kisha nione matokeo yake. Nitakujulisha.--Mwanaharakati (majadiliano) 06:06, 20 Juni 2008 (UTC)
- Bado naona mauzauza (maajabu). Haijakaa sawa bado, lakini wacha nisubiri.
--Mwanaharakati (majadiliano) 06:17, 20 Juni 2008 (UTC)
Nipo katika mashine nyingine naona iko poa wala haina tatizo. Sasa sijui inakuaje ile computer yangu. Lakini poa wacha nisubirie hizo siku mbili moja!--196.41.37.186 10:37, 20 Juni 2008 (UTC)
Greek alphabet
Majadiliano yamehamishwa kwenda Alfabeti ya Kigiriki
"Caucasian Race"
Salam, Kipala. Eti "Caucasian race" ndiyo nini?--Mwanaharakati (majadiliano) 04:06, 21 Juni 2008 (UTC)
- Sina uhakika jinsi ya kutafsiri ipasavyo. Ni dhana inayofanana na "Wazungu". Yaani hoja la kuwa watu wanaoonekana kama watu wengi wa Ulaya pamoja na Waarabu na Wahindi wa Kaskazini kiasili walitokea kwenye Kaukazi na kusambaa Ulaya, eneo la Mediteranea na hadi Uhindi. Wamefanana umbo la uso na fuvo, rangi (kiasi tu kwa sababu watu weupe sana na watu wenye rangi ya kahawia-kahawia walihesabiwa humo). Hali halisi wanasayansi wa leo hawakubali dhana hiyo lakini bado inatumiwa; Nadhani imetumiwa hasa na watu wanaotaka kugawa watu kufuatana na rangi na hawataki kusema "mweupe, mweusi, mjano" kwa sababu hata ugawaji huu unaonekana haufai.
- Mwenyewe nimeshahangaika jinsi gani kutafsiri ile neno "race"; Waswahili wanatumia mara nyingi "rangi" ninavyoona "rangi" haitoshi na dhana la "Wakaukazi" ni mfano mzuri; kwa kutumia "rangi" si rahisi kuelewa dhana hili kwa undani. --Kipala (majadiliano) 06:23, 21 Juni 2008 (UTC)
- Bao hii: Warusi wakiongea "Wakaukazi" wanasemea watu wanaoishi leo huko kama Waarmenia, Waazerbaijan n.k. Waamerika wakisema hivyo watafakari zaidi ile "rangi". --Kipala (majadiliano) 06:27, 21 Juni 2008 (UTC)
- Original human race created 6000 years ago in Eden near Jerusalem when our world was first created, was yellow with red hair (this combination currently doesn't exist), speaking Adamic Proto-Indo-European worldwide. But later since original sin which occured one daynight after creation of Adam and Eve, humanity began to split to many races such as white, yellow, red and brown, and PIE since Babel began to split to many confused tongues. As you see, caucasian race is ONLY one of later confusions, but NOT original worldwide Adamic race. All what I say is revealed by God here in this Catholic private revelation by Anne Catherine Emmerich: http://www.all-jesus.com/scriptures/bible1-4.htm Our redemption, thus eternal goal is returning to original state as it was 6000 years ago. God provided us chance to return to our original Adamic language and our original Catholic faith at once which I documented here: http://www.wikinfo.org/index.php/Adamic_language Of course our current confused multicolored bodies can be reverted to Adamic state only miraculously by God. 79.162.47.125 09:15, 21 Juni 2008 (UTC)
- I am not sure if you understand any Swahili. In fact there is nothing like a "Caucasian" Race. Sister may have used that expression. Nevertheless in doing so she just mirrored an erraneous view of her contemporaries. Usiingize kitu kama hiki katika wikipedia yetu, naomba sana. --Kipala (majadiliano) 10:22, 21 Juni 2008 (UTC)
- I do not understand Swahili at all. I only contribute missing and interesting data. I talked that caucasian race is not important at all, as any other temporary confusions both racial and linguistical, being only post-Adamic intermediate Noahic ancestor of all confused races used by God along with confused languages to stop "unity under devil", (Tower of Babel) but not UNITY UNDER GOD (Catholic Church). Anne Catherine Emmerich is Catholic Saint blessed by Pope John Paul II and never mirrored any errors. She only reused some terms, but with error-free manner. She had miraculous PRIVATE revelation from INFALLIBLE ONE GOD IN THREE PERSONS, thus she is error-free. Adamic race that is yellow with red hair and ceased to exist, HAS NOTHING TO DO with caucasian race, because predates it. English article about Anne Catherine Emmerich presents too God Himself as He revealed Himself in His real Trinitarian Shape to her: http://en.wikipedia.org/wiki/Anne_Catherine_Emmerich Caucasian race in reality is Noah race, from which we all, white, yellow, red and black are descended after Deluge. As you see, whole post-Deluge humanity is caucasian, and not Adamic, because humans survived only in Noah's Ark that stopped at Caucasian Ararat, and died outside Noah's Ark totally. Please notice, that sin of eating fruits (to gain bad+good knowledge) from tree of knowledge of bad and good placed in Eden near Jerusalem was redeemed by Passion of Christ on Tree of Cross too near Jerusalem, because Redemption could be only done as direct and total opposition of original sin. Please note, that Redemption was performed by God by doing good things under hard suffering, being opposite to original sin that was performed by Adam and Eve by doing bad things under soft pleasure. 79.162.47.125 11:11, 21 Juni 2008 (UTC)
- I am not sure if you understand any Swahili. In fact there is nothing like a "Caucasian" Race. Sister may have used that expression. Nevertheless in doing so she just mirrored an erraneous view of her contemporaries. Usiingize kitu kama hiki katika wikipedia yetu, naomba sana. --Kipala (majadiliano) 10:22, 21 Juni 2008 (UTC)
- Original human race created 6000 years ago in Eden near Jerusalem when our world was first created, was yellow with red hair (this combination currently doesn't exist), speaking Adamic Proto-Indo-European worldwide. But later since original sin which occured one daynight after creation of Adam and Eve, humanity began to split to many races such as white, yellow, red and brown, and PIE since Babel began to split to many confused tongues. As you see, caucasian race is ONLY one of later confusions, but NOT original worldwide Adamic race. All what I say is revealed by God here in this Catholic private revelation by Anne Catherine Emmerich: http://www.all-jesus.com/scriptures/bible1-4.htm Our redemption, thus eternal goal is returning to original state as it was 6000 years ago. God provided us chance to return to our original Adamic language and our original Catholic faith at once which I documented here: http://www.wikinfo.org/index.php/Adamic_language Of course our current confused multicolored bodies can be reverted to Adamic state only miraculously by God. 79.162.47.125 09:15, 21 Juni 2008 (UTC)
- Bao hii: Warusi wakiongea "Wakaukazi" wanasemea watu wanaoishi leo huko kama Waarmenia, Waazerbaijan n.k. Waamerika wakisema hivyo watafakari zaidi ile "rangi". --Kipala (majadiliano) 06:27, 21 Juni 2008 (UTC)
Airbus 380
ULIZO:Mie nauliza,naomba unipe wasifu ndege ya abiria aina ya Airbus A380.urefu wake,upana wake,inabeba abiri wangapi,buti yake inaweza kubeba magari madogo mangapi,imetengenezwa na nchi ngapi. ASANTE. MIE MR,FAUSTINE.A.A.ARUSHA-TANZANIA
- Naomba ukitaka kuandika kwenye ukurasa wa majadiliano andika chini ya maandiko mengine usiandike katikati ya majadiliano mengine! Kuhusu Auírbus: Ukisoma Kiingereza basi bofya hapa: . Hatujaanzisha makala hii bado. Magari utakadiria mwenyewe kufuatana na uzito wa gari na uwezo wa kubeba mzigo unaaonyeshwa. --Kipala (majadiliano) 17:56, 22 Juni 2008 (UTC)
Action Concept
Salam nyingi kutoka Dar es Salaam zikufikie Nd. Kipala, huko Ujerumani uliko! Samahani Mzee wangu. Unaweza kupata kaji muda na ukanitafsria makala hiyo?
Sizani kama huifahamu hiyo kampuni. Inashuhurika na mambo ya filamu. Walifanya hii:
Nitashukuru kama utapata muda huo! Ingekuwepo katika Kiingereza, ningefanya mwenyewe, lakini katika en hamna! Kila lakheri..--Mwanaharakati (majadiliano) 05:14, 23 Juni 2008 (UTC)
- Shikamoo Mzee Kipala. Ahksante kwa tafsiri yako. Lakini kuna kitu umesahau kunitafsiria. Ni zile filamu walizotengeneza na kuongoza. Katika de:wiki inaonyesha filamu walizofanya na kuongoza, lakini sijui ni zipi kati ya juu au chini. Nisaidie tena Mzee wangu.--Mwanaharakati (majadiliano) 15:41, 25 Juni 2008 (UTC)
- Sasa orodha ni filamu zote walizotengenezta (ingawa sina uhakika kaka kweli walitengeneza zote au kuchnagia sehemu ya action tu??). Majina ya filamu unaona mwenyewe; vichwa vianmaanisha:
- Fernsehserien Filamu za mfululizo za TV (TV series)
- Fernsehfilme Filamu za TV
- Kinofilme Filamu za sinema
- TV-Magazine SIJUI TV magazine - ni kama programu za TV
- Dokumentarfilm - filamu ya ?? Kiing documentary
- Musikvideo Video ya muziki --Kipala (majadiliano) 21:23, 25 Juni 2008 (UTC)
- Hali yako Mzee wangu, natumai humzima!! Sikumaanisha hivyo. Naomba angalia ukurasa husika wa Action Concept kwa Kiswahili, utaona nimeweka yale maelezo yote yakiwa katika lugha ya Kijerumani. Sasa nataka unidadafulie yale yaliyowekwa. Halafu umeona sasa hivi kila katika kichwa cha makala chini yake kuna maandishi yameandikwa:
- Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru.
Hilo ndilo nililokuwa nalitaka kipindi kileeee!!! Lakini sasa limekuwa! Basi kila lakheri na kompyuta yangu imerudi kama awali. Sikufanya pupa ya kutaka kufanya lolote lile, la. Kwani si ulinishauri au?? Natumani ndivyo na nimetekeleza ushauri wako!!! Kazi njema..--
Vandalism
Fresh user "Future Perfect at Sunrise" is anglican (he is from England, and he is not African) and repeatedly vandalizes both Greek alphabet article and template, showing total disrespect to these sources:
91.94.16.27 18:11, 30 Juni 2008 (UTC)
Too deep revert
I repaired your revert in Greek alphabet article because you removed references to archaic letters. 79.162.1.235 08:17, 1 Julai 2008 (UTC)
Zana za ufundi
- Salam. Eti kumbe kama sio mkabidhi huwezi kusogeza kurasa wala kupakia picha! Picha nakubali ni sawa tu. Lakini kusogeza (hapana). Kwani upo uwezekano wa kukosea jina na ukataka kusawazisha, itakuwaje??--Mwanaharakati (majadiliano) 16:56, 2 Julai 2008 (UTC)
- Salaam, sijaelewa kiini cha tatizo ni nini. Inahusu jambo la alfabeti ya Kigiriki? Au nini?? --Kipala (majadiliano) 19:29, 2 Julai 2008 (UTC)
- Nazungumzia utumiaji wa zana ambazo awali hazikuwa na ulazima wa kutumiwa na mkabidhi. Hapo awali kiungo cha "sogeza" na kupakia faili ilikuwa na haki ya kila mtu katika wiki. Lakini sasa si "kusogeza" wala "kupakia" vyote ni ni haki ya mkabidhi katika kufanya hivyo. Picha ni sawa kwani hata wao huko de:wiki en:wiki na meta wanataka picha zote zipakiwe katika commons!! Basi hata "sogeza??"--Mwanaharakati (majadiliano) 05:29, 3 Julai 2008 (UTC)
- Mambo yale ya amri za kando la ukurasa sijashughulikia. Labda mabadiliko yametokea wakati hizi sehemu za kando zimetafsiriwa. Sijui ni nani aliyeshughulika?? --Kipala (majadiliano) 10:57, 3 Julai 2008 (UTC)
Sijui ni nani. Lakini mabadiliko yote kuhusu Interface yanafanyika katika BetaWiki. Natumai atakuwa Malangali (sina uhakika), kwasababu katika uteuzi wake wa kutaka kuwa mkabidhi alinuiya:
- Najiteua kuwa mkabidhi ili niweze kutafsri mediawiki.
MediaWiki ndiyo kila kitu na huwezi kubadili chochote katika mediawiki kama sio mkabidhi. Binafsi sikupendezewa (wala hata kuvutiwa na utafsiri wa interface katika sw:wiki). Pia sipendi kwenda betawiki kwa kuwa si-mpenzi wa kutafsiri (sana sana template). Baada ya yote, tutaepuka vipi hili la kurudisha "sogeza?" Naona niende meta kuwaeleza juu hili labda tutapata ushauri!! Ama namna gani??--Mwanaharakati (majadiliano) 12:32, 3 Julai 2008 (UTC)
- Naona ni vizuri. --Kipala (majadiliano) 14:15, 3 Julai 2008 (UTC)
- Jamaa anasema eti kila mtumiaji mpya anakuwa hana uwezo wa kupata kitufe cha "sogeza" hadi afikishe siku nne. Hili jibu tayari. Lakini kwangu naona template tittle zinakaa upande! Yaani ukiandika jina la msanii katika template yoyote ya filamu muziki na albamu jina halikai kati, badala yake linakaa kushoto. Sio hizo tu hata zile za kemia pia zinakaa pembeni kasoro ya Uanishaji tu. Je kwako unaona hivyo??--Mwanaharakati (majadiliano) 16:26, 3 Julai 2008 (UTC)
Swali kutoka user:CarlHinton
Hi Kipala,
I see you can speak English better than I can speak Kiswahili. So I write in English, I hope that is okay.
You have been editing pages that I have put up; this is great to see as this is the true spirit of Wikipedia. But I'm not entirely sure what some of your changes are? For example I could not work out the word kidhehebu - what is this language?
Regards
Carl Hinton
- Hi Carl, I prefer that we continue on your user page as I started over there and maybe someone wants to join in so lets keep it at one place. --Kipala (majadiliano) 13:21, 5 Julai 2008 (UTC)
License
Kipala, salam. Naomba msaada wa utafsri wa haki za upakiaji wa picha. Je unashauku juu ya hili? Kwangu naona vibomba (misamiati) mingi imeandikwa katika license hizi, sasa nilikuwa naomba uzitafsiri moja-moja pindi utapoa mda wa kufanya hivyo. License zenyewe ni kama ifuatavyo:
Baada ya hapo unaenda kutasfiri maneno katika mahali pa kuonyeshea license. Huko utakutana na maelezo mbalimbali juu ya haki hizi za picha! Wakati ndiyo huu, naomba niahidi au nijulishe endapo utaona huna muda wa kufanya hivi!!--Mwanaharakati (majadiliano) 14:07, 5 Julai 2008 (UTC)
Re: Karibu
Asante sana. I know very little swahili but I'm studying it and I thought that editing some sw.wikipedia could be useful both for me and the project :-) I'm trying to make edits that I'm confident are correct, but please be patient with any mistake I might make. I think you invited me to ask if I had questions, so here's one for you: how do they call keyboards (music instrument) in swahili? Couldn't find it in online dictionaries. Thanks in advance :-) Moongateclimber (majadiliano) 09:20, 7 Julai 2008 (UTC)
Tafsiri halisi
Salam, Kipala. Naomba nitafsirie maneno haya kwa Kiswahili:
{{Infobox OS version | name = | family = | logo = | logo_size = | screenshot = | caption = | developer = | website = | source_model = | license = | kernel_type = | first_release_date = | first_release_url = | release_version = | release_date = | release_url = | preview_version = | preview_date = | preview_url = | support_status = | other_articles = }}
Nitashukuru endapo utanisaidia kwa hili! Kila lakheri.--Mwanaharakati (majadiliano) 12:55, 10 Julai 2008 (UTC)
- Naomba uongeze mfano wa matumizi yake (ukurasa n.k.). --Kipala (majadiliano) 14:25, 10 Julai 2008 (UTC)
- Basi hapa.--Mwanaharakati (majadiliano) 14:58, 10 Julai 2008 (UTC)
{{{jina}}} | |
Maelezo ya toleo |
Uhindi wa Kiingereza
Hello Kipala, just a quick note: instead of cut&paste-ing text from Uhindi wa Kiingereza to Uhindi ya Kiingereza, and then redirecting, next time I suggest you use the "sogeza" button. This does both things (moves text to a new title and creates a redirect), and also preserves history (which is moved along with the text).
Sorry if I speak english but the concept was too complex for my poor swahili :-) Moongateclimber (majadiliano) 06:41, 11 Julai 2008 (UTC)