Mumbi

Ndege wakubwa wa familia Bucorvidae
Mumbi
Mumbi kaskazi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Bucerotiformes (Ndege kama hondohondo)
Familia: Bucorvidae (Ndege walio na mnasaba na mumbi)
Jenasi: Bucorvus
Lesson, 1830
Ngazi za chini

Spishi 2:

Mumbi, hondo-ardhi au mbizi wa nyika ni ndege wa jenasi Bucorvus, jenasi pekee ya familia Bucorvidae. Wana mnasaba na hondohondo na hadi juzi waliainishwa katika familia Bucerotidae, lakini ndege hawa ni wakubwa sana na hukaa ardhini takriban saa zote. Urefu wao unaweza kufika mita moja na upana wa mabawa mita mbili. Mumbi ni weusi isipokuwa manyoya makuu meupe ya mabawa. Wana ngozi tupu pande zote za macho na koo yao yenye rangi nyekundu na/au buluu.

Spishi zote mbili zinatokea Afrika chini ya Sahara. Hula wadudu wakubwa, makoa, nyungunyungu, mijusi, nyoka na hata kuchakulo na sungura. Jike huyataga mayai 1-3 katika tundu asilia ya mwamba au mti. Hafungwi ndani ya tundu tofauti na spishi za hondohondo. Hata yakiwapo mayai 2 au 3, kinda mmoja tu aishi. Ndugu wa jozi inayozaa husaidia kuwaletea jike na kinda chakula.

Spishi

hariri

Spishi ya kabla ya historia

hariri
  • Bucorvus brailloni (Miocene ya Maroko)