Mustafa Sanalla (مصطفى صنع الله) amewahi kuwa mwenyekiti wa kampuni ya kitaifa ya mafuta ya Libya (NOC) tangu Mei 2014.[1]

Baada ya kupata Shahada ya uhandisi wa kemikali kutoka Chuo Kikuu cha Tripoli mnamo mwaka 1985, Sanalla alijiunga na kampuni ya mafuta na gesi ya Ras Lanuf, tawi la kampuni ya NOC inayoendesha kiwanda cha kusafisha mafuta cha Ras Lanuf nchini Libya.

Sanalla alipandishwa cheo mara kadhaa hadi alipoteuliwa kuwa mwenyekiti wa NOC mnamo mwaka 2014.[2][3]

Kama mwenyekiti, Sanalla amesaidia kudumisha uhuru wa NOC na kuongeza uzalishaji wa mafuta wa nchini Libya, ambao ulikua umevurugika tangu kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Libya mwaka 2011.[4] Sanalla pia anajishughulisha na juhudi za kuvutia uwekezaji wa kimataifa katika sekta ya mafuta na gesi ya Libya.[5]

Julai 13, 2022 uteuzi wa bosi mpya mkuu wa Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta (NOC), kampuni ya umma inayosimamia sekta ya nishati, chanzo kikuu cha fedha za kigeni nchini. Farhat Bengdara, gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Libya, alichukua nafasi ya Mustafa Sanalla.[1]

Marejeo

hariri
  1. https://roscongress.org/en/speakers/sanalla-mustafa/biography/
  2. "The Libya Times - Mustafa Sanalla: The Man Who is Trying to Save Libya's Oil". www.libyatimes.net (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-14. Iliwekwa mnamo 2019-08-14. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)
  3. "Mustafa Sanalla – The Roscongress Information and Analytical System". roscongress.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-14. Iliwekwa mnamo 2019-08-14.
  4. "Libyan oil chief warns renewed fighting threatens production", Financial Times, 11 April 2019. 
  5. "Sanalla holds Houston meetings in US$ 60-billion procurement drive to increase Libya's oil production to 2.1 mbpd by 2023". Libya Herald (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-22. Iliwekwa mnamo 2019-08-14.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mustafa Sanalla kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.