Tripoli, Libya

(Elekezwa kutoka Tripoli (Libya))


Kwa miji mingine inayoitwa "Tripoli" tazama makala ya maana Tripoli

Jiji la Tripoli
Nchi Libya
Mahali ilipo Tripoli katika ramani ya Libya.

Tripoli ni mji mkuu wa Libya.

Jina la Kiarabu ni طرابلس (tarāblus) au طرابلس الغربية (tarābulus al-gharbiyya - Tripoli ya Magharibi kwa sababu ya Tripoli ya mashariki huko Lebanon) lina asili ya lugha ya Kigiriki (Τρίπολη) likimaanisha "miji mitatu".

Tripoli ina wakazi 1,150,990 ambayo ni zaidi ya robo moja ya wakazi wote wa Libya na inaendelea kukua haraka.

Jiji hilo liko ufukoni mwa bahari ya Mediteranea likiwa na hali ya hewa ya wastani. Mwezi Agosti inafika halijoto ya sentigredi 28,1°, Januari sentigredi 12,1°. Miezi ya baridi kuna mvua, Juni hadi Agosti ni majira ya kiangazi.

Tripoli ina bandari kubwa kabisa ya Libya na pia ni kitovu cha serikali, biashara na viwanda.

Tripoli ni mji wa kale ambao bado historia yake imetunzwa ikionyesha mabaki ya historia yake ndefu tangu enzi za Wafinisia, Waroma, Waarabu, Wahispania, Waturuki na Waitalia.

Picha za Tripoli

hariri

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tripoli, Libya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.