Muundo katika lugha ni mpangilio na mtiririko wa visa na matukio katika kazi ya kifasihi. Hapa tunachunguza jinsi msanii wa kazi hiyo alivyounda na alivyounganisha tukio moja na jingine, kitendo kimoja na kingine, sura moja na nyingine. Tunapohakiki muundo katika kazi ya kifasihi, hasa riwaya na tamthilia, kuna mambo ya kuzingatia. Mambo hayo ni:

  • Aina ya muundo
  • Mgawanyo wa kazi hiyo
  • Umbo la kazi hiyo

Aina za muundo

hariri
  • Kuna aina tatu za muundo. Aina hizo ni:

Muundo msago

hariri
  • Huu ni muundo wa moja kwa moja ambao visa na matukio vimepangwa katika hali ya kufuatana kuanzia tukio la kwanza hadi la mwisho.

Muundo rukia

hariri
  • Ni aina ya visa na matukio. Hapa kunakuwa na visa viwili au zaidi ambavyo hurukiana katika kusimuliwa kwake na mwisho wa visa hivyo hugawana na kuwa kisa kimoja.

Muundo changamano

hariri
  • Huu ni muundo ambao kunakuwa na muundo wa msago na rukia. Hapa visa huanza kwa urejeshi na kumaliziwa na msago.

Mgawanyo wa kazi hiyo

hariri

Katika mgawanyo wa kazi mhakiki anapaswa kueleza:

  • Sura/namba=riwaya
  • Sehemu/onesha=tamthiliya
  • Idadi ya mistari kwa ubeti=ushauri

Ikumbukwe kwamba mwandishi anaweza kugawa kazi yake katika sehemu lakini akaipa picha sura na taswira.

Umbo la kazi hiyo

hariri

Katika kuangalia umbo la kazi mhakiki anapaswa kueleza kama kazi hiyo ni riwaya tamthiliya au ushairi.

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Muundo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.