Muungano wa Madola ya Afrika

Muungano wa Madola ya Afrika ni wazo lililopendekezwa kwa ajili ya shirikisho la baadhi ya nchi zote huru 54 za katika bara la Afrika.

Ramani ya nchi huru 54 za Afrika jumlisha eneo lililokuwa na mgogoro la Sahara Magharibi

Wazo hili linatokana na shairi la Marcus Garvey la mwaka wa 1924, Hail, United States of Africa.[1][2]

Kiongozi wa zamani wa Libya Muammar al-Gaddafi, ambaye 2009 alikuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA), aliendeleza wazo la Muungano wa Madola ya Afrika katika mikutano mwili ya kanda ya Afrika: wa kwanza mwezi Juni 2007 mjini Conakry, Guinea,[3] halafu tena mnamo mwezi wa Februari mwaka 2009 mjini Addis Ababa, Ethiopia.[4] Gaddafi awali alisukuma kuanzishwa kwa suala hili katika mkutano uliofanyika mwaka 2000 mjini Lomé, Togo,[5] aliealeza UA kama kushindwa kwa baadhi ya mambo; Gaddafi alidai ya kwamba muungano wa kweli pekee ndiyo unaweza kutupatia uthabiti na utajiri kwa Afrika yetu. Baadhi ya viongozi wakuu wa UA walikubaliana na shirikisho lililopendekezwa, wakiamini ya kwamba ingeliweza kuleta amani katika Afrika mpya.[6] Alpha Oumar Konaré, Rais wa zamani wa Mali na mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Umoja wa Afrika, alizungumzia wazo hili katika sherehe za Siku ya Afrika, mnamo Mei 25, 2006.[7]

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Ambitious plan for a new Africa: Welcome to the U.S.A (that's the United States of Africa)". The Independent. 30 Juni 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-13. Iliwekwa mnamo 2009-04-26.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Thabo Mbeki (9 Julai 2002). "Launch of the African Union, 9 July 2002: Address by the chairperson of the AU, President Thabo Mbeki". ABSA Stadium, Durban, South Africa: africa-union.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-03. Iliwekwa mnamo 8 Februari 2002.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Gaddafi Calls for a "U.S." of Africa, from Mafé Tiga blog, July 1, 2007
  4. AU summit extended amid divisions, from BBC News, 4 February 2009
  5. "United States of Africa?", from BBC News, 11 July 2000
  6. Gaddafi urges pan-African state, from BBC News, 26 June 2007
  7. "Statement of the UA Commission Chairperson". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-29. Iliwekwa mnamo 2015-06-20.