Mwangata
Mwangata ni kata ya Manisipaa ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Tanzania yenye Postikodi namba 51112.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 24,673 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,486 waishio humo.[2]
Jina Mwangata linasemekana lilitokana na uwepo wa mzee mmoja mtaalamu wa jadi katika eneo hilo. Mzee huyo alikuwa akitoa tiba yake kwa mfumo wa pekee kwani alikuwa akichukua vijiti vidogovidogo pamoja na magome halafu alifunga kama 'ngata' ya kubebea kuni/maji ambayo kwa lugha asilia ya Kihehe inaitwa ng'ata. Hivyo basi wanakijiji walikuwa wakisema kuwa wanakwenda kwa mtaalamu "mwangata" na jina hilo likapata umaarufu mkubwa na mpaka sasa bado linatumika. [3]
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ Sensa ya 2012, Iringa Region- Iringa Municipal Council
- ↑ Maelezo haya yaliletwa na mtumiaji asiyejandikishe akijitambulisha ni Wilson Semba wa Mwangata 'D'
Kata za Wilaya ya Iringa mjini - Tanzania | ||
---|---|---|
Gangilonga | Igumbilo | Ilala | Isakalilo | Kihesa | Kitanzini | Kitwiru | Kwakilosa | Makorongoni | Mivinjeni | Mkimbizi | Mkwawa | Mlandege | Mshindo | Mtwivila | Mwangata | Nduli | Ruaha |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mwangata kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |