Mkoa wa Iringa ni mojawapo kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye Postikodi namba 51000. Upo katikati ya nchi, kidogo upande wa kusini. Umepakana na mikoa ya jirani ya Morogoro, Njombe, Mbeya, Singida na Dodoma.

Mahali pa Mkoa wa Iringa katika Tanzania.
Mji wa Iringa.

Makao makuu yako katika manisipaa ya Iringa.

Jiografia Edit

Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania na kupakana na ukanda mkavu wa kati wa Tanzania upande wa kaskazini.

Hadi mwaka 2012 Mkoa wa Iringa ulikuwa na eneo lenye ukubwa wa jumla ya km² 58,936. Wastani wa asilimia 74 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo ambalo ni sawa na km² 43,935. Eneo linalobakia la km² 15,001 ni eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama milima na misitu.

Tangu mwaka 2012 wilaya tatu za kusini zimetengwa na Iringa na kuwa mkoa mpya (Mkoa wa Njombe) kwa hiyo eneo la Iringa limepungua kilomita za mraba 21,347.

Wakazi Edit

Mwaka 2022 kulikuwa na wakazi 1.192,728 [1] katika wilaya zifuatazo: Iringa Vijijini (wakazi 254,032), Mufindi (wakazi 265,829), Kilolo (wakazi 218,130), Iringa Mjini (wakazi 151,345), na Mafinga Mjini (wakazi 51,902).

Wenyeji wa mkoa ni hasa Wahehe; wengine wanatokea makabila ya jirani kama Wabena, Wakinga, Wapangwa, Wasangu, Wawanji, Wagogo n.k.

Majimbo ya bunge Edit

Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:

Tazama pia Edit

Marejeo Edit

  1. https://assengaonline.com/2022/11/05/matokeo-ya-sensa-2022-tanzania/

Viungo vya nje Edit