Mwendamaji
Mwendamaji (Gerris thoracicus)
Mwendamaji (Gerris thoracicus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda ya juu: Paraneoptera
Oda: Hemiptera
Haeckel, 1896
Nusuoda: Heteroptera
Oda ya chini: Gerromorpha
Familia ya juu: Gerroidea
Familia: Gerridae
Leach, 1815
Ngazi za chini

Nusufamilia 8:

Wendamaji au watembeaji-maji ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa familia Gerridae katika oda ya chini Gerromorpha ya oda Hemiptera na nusungeli Pterygota (wenye mabawa) ambao hutembea juu ya maji na kujilisha kwa wadudu walioanguka majini au wanaokuja usoni kwa maji ili kupumua (k.m. lava wa mbu).

Takriban spishi zote zinatokea juu ya maji baridi lakini spishi fulani katika jenasi Asclepios, Halobates na Stenobates huishi juu ya maji ya bahari (kunguni-bahari). Hata katika familia za Hermatobatidae na Veliidae kuna spishi kadhaa kama hizi. Kwa kawaida hukaa karibu na pwaa lakini spishi tano za Halobates huishi mbali na pwaa kwenye bahari wazi. Hawa ni wadudu pekee wa makazi haya.

Maelezo

hariri

Wendamaji wana mwili uliorefuka na miguu mirefu ya kati na ya nyuma. Sifa nyingine ni kucha nyuma ya ncha za miguu zinazoweza kukunjwa na nywele za kukwepa maji. Nywele hizo ni ndogo sana na zina msongamano wa zaidi ya elfu moja kwa mm. Mwili mzima umefunikwa na nywele, ambayo inapatia mwendamaji mkinzano dhidi ya kurusha au matone ya maji. Kwa kuwa nywele hufukuza maji, huzuia matone kwa kuelemea mwili.

Wadudu hao kwa ujumla ni wadogo wenye miguu mirefu na urefu wa mwili wa spishi nyingi ni kati ya mm 2 hadi 12. Wachache ni kati ya mm 12 na 25. Spishi moja, Gigantometra gigas, ya mito kwenye kaskazini kwa Vietnam na kusini tangamani kwa Uchina, isiyojulikana sana, inaweza kufikia mm 36 na kuwa na miguu ya kati na ya nyuma ambayo inazidi sm 10 kila mmoja. Baina ya jenasi zilizoenea, Aquarius ina spishi kubwa zaidi ambazo kwa ujumla huzidi mm 12, angalau majike, na spishi kubwa kabisa ni mm 24 kwa wastani. Kwa kawaida majike huwa wakubwa kwa wastani kuliko madume wa spishi zao, lakini inaonekana kugeuzwa katika Gigantometra gigas, ambayo kwa kawaida hufikia urefu wa mwili wa mm 36 kwa madume wasio na mabawa na mm 32 kwa majike wenye mabawa (madume wenye mabawa, hata hivyo, ni wakubwa kidogo tu kwa wastani kuliko majike).

Wendsmaji wana vipapasio vyenye pingili nne kila kimoja. Pingili hizi zinahesabiwa kutoka karibu na kichwa hadi ncha. Pingili ya tatu ina nywele fupi na ngumu. Kulingana urefu wa pingili za vipapasio kunaweza kusaidia kutambua spishi za kipekee ndani ya familia Gerridae, lakini kwa kawaida pingili ya kwanza ni ndefu na nene kuliko zile tatu nyingine. Pingili nne zilizojumuishwa sio ndefu kuliko urefu wa kichwa kwa kawaida.

Kidari cha wendamaji kwa ujumla ni kirefu na chembamba. Mara nyingi urefu wake ni kutoka mm 1.6 hadi 3.6 baina ya spishi zote na miili fulani ni ya mcheduara au ya mviringo zaidi kuliko mingine. Pronoto inaweza kung'aa au la kulingana na spishi na kufunikwa kwa nywele ndogo sana ili kusaidia kukwepa maji. Fumbatio ina pingili kadhaa na kuwa na metasterno yenye vidomo vya tezi ya harufu.

Miguu ya mbele ni mifupi na ina kucha zilizotoholewa ili kutoboa mbuawa. Miguu ya kati ni mirefu kuliko jozi ya kwanza lakini mifupi kuliko ile ya mwisho. Imetoholewa kwa kujisogeza juu ya maji. Miguu ya nyuma ni mirefu kuliko yote mingine na hutumika ili kutanda uzito wa mdudu kwenye eneo kubwa la uso wa maji na pia kuendesha mdudu kupitia uso wa maji. Miguu ya mbele imeunganishwa karibu na macho lakini miguu ya kati ni karibu zaidi na ile ya nyuma iliyopo katikati ya kidari na kuenda mpaka nyuma ya ncha ya fumbatio.

Spishi za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Aquarius distanti
  • Eurymetra angolensis
  • Eurymetra natalensis
  • Eurymetra nitidula
  • Gerris gobanus
  • Gerris hypolence
  • Gerris swakopensis
  • Gerris zuqualanus
  • Limnogonus capensis
  • Limnogonus curriei
  • Limnogonus cereiventris
  • Limnogonus hypoleucus
  • Limnogonus intermedius
  • Limnogonus nigrescens
  • Limnogonus poissoni
  • Halobates alluaudi
  • Halobates flaviventris
  • Halobates germanus
  • Halobates hayanus
  • Halobates micans
  • Halobates poseidon
  • Naboandelus africanus
  • Naboandelus bergevini
  • Naboandelus hynesi
  • Neogerris severini
  • Rhagadotarsus hutchinsoni
  • Tenagogonus albovittatus
  • Tenagometra hirsuta
  • Tenagometra lanuginea

Kutazama

hariri

Wendamaji wakiwinda

  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwendamaji kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.