My Life
"My Life" ni kibao cha tatu cha rapa The Game kutoka katika albamu yake ya tatu, LAX ambao ilitolewa mnamo tar. 22 Agosti 2008. Wimbo umetayarishwa na Cool na Dre, ukimshirikisha Lil Wayne, na ipo kama jinsi nyimbo zake nyingi za karibuni alizotoa Lil Wayne, anatumia kionjo cha Auto-Tune kwa ajili ya kiitikio.
“My Life” | |||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Single ya The Game akimshirikisha Lil Wayne kutoka katika albamu ya LAX | |||||||||||
Imetolewa | 22 Julai 2008 (U.S.) 5 Agosti 2008 (iTunes) | ||||||||||
Muundo | CD single Digital Download | ||||||||||
Imerekodiwa | 2008 | ||||||||||
Aina | West Coast hip hop, Hip hop | ||||||||||
Urefu | 5:27 (album version)[1] 4:35 (extended radio edit)[1] 3:38 (main radio edit)[1] | ||||||||||
Studio | Geffen/Interscope | ||||||||||
Mtunzi | Jayceon Taylor Dwayne Carter, Jr. | ||||||||||
Mtayarishaji | Cool na Dre | ||||||||||
Mwenendo wa single za The Game akimshirikisha Lil Wayne | |||||||||||
|
Historia
haririKurekodi
haririWatayarishaji Cool na Dre wametoa makala ya video yanayoonyesha namna walivyotengeneza biti la wimbo huu.[2]
The Game alizungumza juu ya kazi yake waliyofanya na Lil Wayne na kueleza:
Unapokuwa ndani ya studio na Wayne, unaweza kutulia sana yaani, mshikaji, kwa sababu kila kitu kina kuwa rahisi kinoma. Anaweza kwenda na mamelodi ajabu. Pindi apigapo na ma-idea, au niibuke na ma-idea, tunanyoosha, mwana. Mchakato wake ni rahisi. Ninafikiri mimi na yeye labda tungeweza kufanya albamu, kama, sikui saba hivi. Albamu bab-kubwa! Anaiwekea 100, naiwekea 100. Sote ni Ma-MC wenye vipaji. Nakumbali sana kwenye hip-hop.[3]
Nafasi ya chati
hariri"My Life" ilitolewa kwa mara ya kwanza kupiti maduka ya iTunes huko Amerika ya Kaskazini kwa ajili upakuaji wa dijitali. Nchini Marekani, iliingia kwa kushika nafasi ya #21 kwenye chati za Billboard Hot 100 inaifanya kuwa kibao pekee cha The Game kushika nafasi ya juu sana kwenye chati. Pia iliingia na kushika nafasi ya #32 kwenye Pop 100 ambayo pia inashughulika na masuala ya upakuaji mkondoni. Huko nchini Kanada iliingia na kushika nafasi ya #42 kwenye chati za Canadian Hot 100 na wiki hiyohiyo pia ikaingizwa kwenye orodha upakuaji mkondoni. Kwenye chati za UK Singles Chart ma kushika nafasi ya #34.
Chati (2008) | Nafasi iliyoshika |
---|---|
Canadian Hot 100[4] | 42 |
U.S. Billboard Hot 100[5] | 21 |
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs | 15 |
U.S. Billboard Hot Rap Tracks | 4 |
U.S. Billboard Mainstream R&B/Hip-Hop | 9 |
U.S. Billboard Pop 100 | 32 |
Irish Singles Chart | 32 |
Swiss Singles Chart | 49 |
UK Singles Chart[6] | 34 |
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 According to single cover.
- ↑ 305 Uncut Presents Making The Beat Cool & Dre "My Life" Part 1 Ilihifadhiwa 12 Septemba 2008 kwenye Wayback Machine. Accessed 23 Agosti 2008.
- ↑ Andres Tardio (18 Agosti 2008) Why Did Game Say "Hip Hop Broke My Heart?" Ilihifadhiwa 5 Januari 2009 kwenye Wayback Machine. HipHopDX. Accessed 21 Agosti 2008.
- ↑ "Billboard Canadian Hot 100". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-21. Iliwekwa mnamo 2009-12-29.
- ↑ "Billboard.com - Artist Chart History - The Game". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-08-22. Iliwekwa mnamo 2008-08-22.
- ↑ The Official UK Charts Company: TOP 100 SINGLES CHART