Duma (Siri ya Mtungi)

Duma ni jina la uhusika kutoka katika tamthilia ya Siri ya Mtungi kutoka nchini Tanzania. Uhusika umechezwa na Daudi Tairo. Duma ni mtoto wa mjini, kazi yake hasa ni u-DJ katika kumbi za muziki na sherehe mbalimbali za vigodoro na mambo mengine. Vilevile ni mtu wa mipango ya mjini (misheni-tauni), hasa mipango hiyo hufanya na Mzee Masharubu akiwa na kijana wake mtiifu wa Masharubu, Kovu. Mara kadhaa amekuwa akipokea mizigo ya magendo kutoka pwani ya Zanzibar na kuisambaza sehemu mbalimbali. Kazi hii ni pasua kichwa kwake, hasa ukizingatia bosi wa kazi hizo ni Masharubu na hakuna mtu mdhulumati kama Masharubu. Pamoja na magumu yote, bado alitumia nguvu kwa hali na mali, aidha kihalali ama si kihalali kujipatia kipato.

Duma
muhusika wa Siri ya Mtungi

Taswira ya Duma (Siri ya Mtungi) (uhusika umechezwa na Daudi Tairo)
Imebuniwa na MFDI Tanzania
Imechezwa na Patrick Masele
Idadi ya sehemu 26
Misimu
1, 2
Maelezo
Jinsia Kiume
Kazi yake DJ, mwuza madawa ya kulevya, misheni-tauni
Ndugu Steven
Dini Mkristo
Utaifa Mtanzania

Mara kadhaa ameonekana kujutia nafsi yake kwa kujihusisha na shughuli za kitapeli na mali za magendo na mihadarati, lakini shida na hanasa za maisha zinamfanya akose misimamo thabiti na kuendelea upande wa pili. Aliweza kumwambia Masharubu hataki mali zake za magendo, lakini alishindwa kumkatalia Golden na Ish mipango yao ya uingizwaji wa dawa za kulevya mjini Bagamoyo na kuzileta eneo la Dar es Salaam. Duma ana mahusiano ya kimapenzi ya dhati na Nusura, lakini vilevile ana mahusiano na wanawake wengine kibao huko vilabuni. Vilevile aliwahi kuishi kinyumba na Rose mwishowe akamwingiza mjini kwa kumlengesha kwa maaskari na kumwacha akiwa apeche alolo. Sifa kubwa ya Duma ni kutokubali kushindwa na mapenzi ya hali ya juu kwa mdogo wake Steven.[1]

Muhtasari wa sehemu ya kwanza mpaka sehemu ya kumi na tatu hariri

Duma ni mmoja wa wahusika wakuu katika tamthilia ya televisheni inayoitwa “Siri ya Mtungi”. Duma ni DJ na ana kaka mdogo, Steven, ambaye anamtazama kama mtu wa kuigwa. Kwenye sehemu hadi sasa, hawajawataja wazazi wa Duma na Steven. Tunachokiona ni kwamba, Duma anajitahidi kusimamia maisha yake pamoja na kumtunza mdogo wake, Steven. Tunaona pia kuwa Duma anatembelea kwa siri upendo wake, Nusura, wakati baba ya Nusura hayuko. Duma anataka kuwa na Nusura lakini Nusura anaogopa kwamba baba yake atakataza uhusiano huo. Katika sehemu ya tatu, Duma amegundua kuwa Steven amekuwa mwanafunzi mbaya, hutoroka darasani, hafanyi kazi zake za shule, na hafaulu mitihani yake. Duma alimsihi mkuu wa shule kumpa Steven nafasi ya pili. Mwalimu mkuu anakubali kufanya hivyo, lakini sio kabla ya kumwambia Duma kwamba kuna wanafunzi wengi ambao wanataka kupata nafasi ya Steven katika shule hiyo. Mwalimu mkuu pia anahoji uwezo wa Duma wa kuwa mfano wa kuigwa na Steven na anasema kuwa pesa haisuluhishi shida zote. Wakati Duma anakabiliana na Steven, Steven anamwambia kaka yake kwamba anasikitika sana na kwamba anataka kufuata njia ya Duma kama DJ. Duma anahisi kuwa na hatia na anamsamehe Steven, akimwambia kwamba elimu itafungua milango ya fursa nyingi. Katika sehemu ya nne, Duma anatembea ndani ya nyumba yake na kuona kwamba Steven ana msichana kitandani pamoja naye. Duma anakasirika sana na anamwonya Steven kwamba anaweza kupata magonjwa ya zinaa ikiwa hajilindi. Duma basi anapendekeza kuwa Steven anapaswa kuishi na mtu mwingine kwa sababu Duma anaamini kwamba yeye ni mfano mbaya kwa Steven. Katika sehemu ya kumi na moja, mkuu wa shule anamjulisha Duma kwamba Steven amefukuzwa katika shule hiyo. Duma basi anagundua kuwa Steven ana magonjwa ya zinaa. Wakati Duma anagundua kuwa Nusura anaolewa na Mzee Kizito, alikuwa na huzuni sana. Katika sehemu ya saba, Duma anakutana na Nusura siku ya harusi yake, akamuuliza kwanini aliamua kuolewa na Mzee Kizito. Duma anashindwa kumshawishi Nusura aache harusi hiyo. Masharabu, baba ya Nusura, anamkuta Duma hapo na anamlazimisha Duma aondoke na walinzi wake. Tunaona kwamba Duma anasumbuka sana baada ya harusi na mara nyingi anaenda kwenye baa kuwachukua wanawake kulala naye na kupigana na watu wengine. Katika sehemu ya kumi na moja, Nusura anagundua kuwa ni mjamzito na anaamini kuwa Duma ndiye baba wa mtoto. Wakati mwingine kwamba Duma anamzungumzia na Nusura alikuwa katika sehemu ya kumi na tatu. Duma anamwona Nusura akitembea barabarani na anapata tahadhari yake. Duma anamzungumza kwamba furaha maishani yake na anamkumbusha kwamba harusi ilikuwa kosa, lakini Nusura hakubaliani na anamambia kuwa kila mtu hufanya furaha yao wenyewe. Bado Duma anaamini kwamba waliumbwa kwa kila mmoja kuoa na kupata watoto pamoja. Nusura anatembea mbali naye na hakumwambia juu ya mtoto kuwa wake. Itaendelea.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Duma (Siri ya Mtungi) Archived 12 Septemba 2016 at the Wayback Machine. katika wavuti rasmi ya Siri ya Mtungi.