NRC Handelsblad, mara nyingi hufupishwa kuwa NRC, ni gazeti la kuchapishwa kila siku.Gazeti hili huchapishwa jioni katika nchi ya Uholanzi na Kampuni ya NRC Media. Gazeti hili liliumbwa mnamo 1 Oktoba 1970 kutokana na muungano wa jarida la Nieuwe Rotterdamsche Courant na jarida la Algemeen Handelsblad.Jarida la Algemeen Handelsblad llikuwa jarida kuhusu hesabu za kibiashara kwa jumla na jarida la Nieuwe Rotterdamsche Courant lilikuwa gazeti la Roterdam. Katika mwaka wa 2006, jarida la porojo, nrc•next, lilianza kuchapishwa. Katika mwaka wa 2007, usambazaji wa NRC Handelsblad ulikuwa nakala 249,099 katika siku ya Jumatatu hadi Ijumaa na nakala 270,189 katika siku ya Jumamosi.

NRC Handelsblad
Jina la gazeti NRC Handelsblad
Aina ya gazeti *.Gazeti la kila siku
*.Lugha ya Kiholanzi
*.57 cm x 41.5 cm
Lilianzishwa 1970
Nchi Uholanzi
Mhariri Peter Vandermeersch
Makao Makuu ya kampuni *.Marten Meesweg 35
*.Rotterdam
Nakala zinazosambazwa *.244,099 Jumatatu - Ijumaa
*.270,189 Jumamosi[1]
Tovuti http://www.nrc.nl

Historia hariri

Gazeti la NRC Handelsblad lilianzishwa mnamo 1 Oktoba 1970, baada ya muungano wa gazeti la Amsterdam la Algemeen Handelsblad na gazeti la Rotterdam la Nieuwe Rotterdamsche Courant. Nieuwe Rotterdamsche Courant lilianzishwa katika mwaka wa 1844 na Henricus Nijgh huko Rotterdam. Gazeti la Algemeen Handelsblad lilianzishwa katika jiji kuu la Amsterdam katika mwaka wa 1828 na J.W. van den Biessen. Wito wa jarida hili,NRC Handelsblad ni Lux et Libertas- hasa ukimaanisha Mwangaza (ikiashiria wakati wa kuzuzuliwa na kuerevushwa- yaani mwangaza unawafungua macho) na Uhuru.

Usambazaji wa gazeti hili ulikuwa nakala 242,950 katika mwaka wa 2004(idadi chache kuliko usambazaji wa nakala 265,000 katika mwaka wa 2002). Jumla ya usambazaji wa magazeti ulikuwa 4,013,547 katika mwaka wa 2004.

Katika mwezi wa Februari 2006,NRC Handelsblad ilianzisha gazeti dogo la asubuhi la kuvutia wasomaji wasomi ambao hawawezi kusoma gazeti la kila siku. Mhariri Folkert Jensma alipoondoka, nafasi yake ilichukuliwa na Birgit Donker mnamo 12 Desemba 2006.

Mtindo wa uchapishaji hariri

Tangu mwaka wa 2001, mtindo wa Lexicon umetumika. Mtindo huu wa uchapishaji uliandaliwa na Bram de Does na hutumika katika gazeti hili. De Does alichora na kuandaa mtindo maalum ya kutumika katika kuchapisha vichwa vya habari motomoto.

Viungo vya nje hariri

Marejeo hariri

  1. Egeria in an investment company which is part of Bregal Investments, which is part of Cofra Group
  2. NRC Handelsblad 12 December 2006 page 21 Tegenwicht aan Trivialisering: Birgit Donker benoemd tot hoofdredacteur van NRC Handelsblad"Birgit Donker is de nieuwe hoofdredacteur van NRC Handelsblad, nrc.next en nrc.nl. De raad van bestuur van PCM heeft haar vandaag benoemd. Rotterdam, 12 Desemba Birgit Donker (41) is de opvolger van Folkert Jensma als hoofdredacteur van NRC Handelsblad."