Nanomita

Nanomita (ing. nanometer, alama nm[1]) ni kipimo cha SI cha kutaja urefo mdogo wa 10−9 mita. Kwa lugha nyingine, ni sehemu ya bilioni 1 ya mita 1.

MatumiziEdit

Kipimo hiki hutumiwa kwa kutaja vipimo katika fizikia ya atomi na molekuli, pia katika biolojia kwa vipimo vya kiini cha seli na jenetikia. Kipenyo cha atomi ya heli ni takriban 0.1 nm; virusi nyingi vina kipenyo cha baina 20 nm na 300 nm.

Nanomita ni pia kipimo cha kawaida kwa kutaja urefu wa mawimbi ya usumakuumeme. Nuru inayoonekana ina urefu wa wimbi kati ya 400 nm hadi 800 nm. .[2]

Kipimo hiki kinatumiwa sana kwa makadirio katika teknolojia ya nano.

Neno latokana na lugha ya (Kigiriki: nanos (νάνος, "kibete") pamoja na neno "mita" (gir.μέτρον, metrοn, "kizio cha kipimo")

UlinganifuEdit

Nanomita 1 = 1.0 x 10−9 mita = 1000 pikomita; 1000 nm = 1 mikromita

MarejeoEdit

  1. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-06-10. Iliwekwa mnamo 2015-06-07.
  2. Hewakuruppu, Y., et al., Plasmonic “ pump – probe ” method to study semi-transparent nanofluids, Applied Optics, 52(24):6041-6050

Tazama piaEdit

MarejeoEdit


Tovuti za NjeEdit