Natasha Sutherland

Mwigizaji wa kike kutoka Afrika Kusini

Natasha Sutherland amezaliwa Durban, Afrika Kusini,tarehe 20 Novemba mwaka 1970) ni mwigizaji wa Afrika Kusini. Anajulikana zaidi kwa majukumu yake katika vipindi vya maigizo katika runinga ikiwemo Honeytown, Tarzan: The Epic Adventures na Scandal!. Mbali na kuigiza, yeye pia ni mwandishi, msemaji wa kuhamasisha na mshauri.[1]

Maisha binafsi hariri

Alizaliwa Novemba 20 mwaka 1990 kama Binti wa choreographer Geoffrey Sutherland na Ken Lynn Ashby.[2]

Alikuwa ameolewa na Steve Hofmeyr, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, na mtangazaji wa runinga wa Afrika Kusini.[3].Walioana mnamo mwaka 1998 na baadaye waliachana mnamo mwaka 2008, chanzo kikiwa ni uhusiano mwingine uliodumu kwa miaka 10 baina ya Steve na mkufunzi wa mazoezi ya mwili Janine van der Vyver.[4].Wanandoa hao wana watoto wawili Benjamin na Sebastian.[5]

Kazi hariri

Alianza kazi yake mwanzoni mwa miaka ya 1990 kama mtangazaji wa kipindi cha watoto katika televisheni. Kisha akaigiza katika telenovela, filamu ya Egoli: The Place of Gold wakati wa ujana wake mnamo mwaka 1991. Mnamo mwaka 1996, alianza kazi yake ya uigizaji na filamu mbili za runinga ikiwemo "Honeytown" na Tarzan: The Epic Adventures. Baada ya kufanikiwa katika filamu hizo, aliigiza katika sinema ya nyumbani Operational Delta mnamo mwaka 1997. Wakati huo huo, alianza kutawala katika kumbi za michezo ya kuigiza ya Afrika Kusini na michezo kadhaa maarufu kama "Gigi" ya mwaka 1992 na The Revlon Girl. Wakati huo huo, pia aliongoza video za muziki na alifanya kazi kama mhariri wa Jarida la Finesse.[2]

Mbali na kuigiza, Natasha pia ni mhamasishaji wa umma ambaye alisafiri kote nchini na pia katika ngazi ya kimataifa. Ameteuliwa pia kama balozi wa chapa ya Urembo ya Afrika Kusini Placecol na DNB. Yeye pia ni mwandishi hodari, ambaye aliandika kitabu chake cha kwanza "Bittersweet". Pamoja na mafanikio yake kama mwandishi, baadaye aliandika vitabu kama: "Green and Blue" mwaka 2010, "Fairytale" na "Sprokie".[2]

Filamu hariri

Mwaka Filamu Uhusika Aina Marj.
1991 Egoli: Place of Gold Samantha Ryan du Plessis Filamu za Televisheni
1994 Honeytown Carrie Filamu za Televisheni
1995 Honeytown II Carrie Filamu za Televisheni
1995 The Uninvited Guest Mandy Thompson Filamu za Televisheni
1997 Tarzan: The Epic Adventures Dalen Filamu za Televisheni
1997 Operation Delta Force Lt. Marie Junger Filamu
1998 Wycliffe Young Mum Filamu za Televisheni
2008 Scandal! Layla McKenzie Filamu za Televisheni


Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Natasha Sutherland kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.