Ndegesukari
Ndegesukari | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Ndegesukari wa rasi
| ||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
|
Ndegesukari (kutoka Kiing.: sugarbird) ni ndege wa familia Promeropidae. Wanatokea Afrika Kusini tu. Domo lao limepindika na mkia ni mrefu sana, kwa dume hasa. Ulimi wao ni mrefu wenye ncha kama brashi na unaweza kuchomozwa nje ili kula mbochi. Hupata nguvu yao takriban yote kutoka mbochi wa maua ya jenasi Protea na ndege hawa ni wachavushaji muhimu wa maua haya. Hula pia wadudu ambao wanavutika na maua ya Protea, kama nyuki na nzi. Hulijenga tago lao katika panda ya mti na jike huyataga mayai mawili.
Spishi za AfrikaEdit
- Promerops gurneyi, Ndegesukari-milima (Gurney's Sugarbird)
- Promerops cafer, Ndegesukari wa Rasi (Cape Sugarbird)