Ndoto ya Amerika ni kitabu cha watoto kilichoandikwa na Ken Walibora. Ken Walibora alikuwa mwandishi maarufu wa Kenya ambaye alifanya kazi na kuandika zaidi ya vitabu ishirini na kushinda tuzo nyingi kwa kazi yake. Alishinda Tuzo ya Fasihi Jomo Kenyatta mara mbili kwa Ndoto ya Amerika mwaka wa 2003 na Kisasi Hapana mwaka wa 2009.

Hii ni picha ya Ken Walibora. Alizaliwa mwaka 1965 huko Baraki, Bungoma, Kenya.
Jalada la kitabu, Ndoto ya Amerika. Picha ya jalada la kitabu ni ya Isaya chini ya mganga.* Alipotorokea msituni, analala chini ya mti na ana ndoto yake ya kwanza kuhusu Amerika.

Utangulizi

hariri

Kitabu hiki kinaelezea maisha ya Isaya Yano. Isaya ndiye mhusika mkuu wa kitabu. Kitabu hicho pia kinaonyesha maisha ya rafiki mkubwa wa Isaya, Madoa. Mandhari ya hadithi hii ni nchini Kenya. Isaya anaishi Sangura katika tarafa ya Cherangani, Wilayani Trans-Nzoia. Isaya na Madoa wote ni wavulana masikini wa mashambani ambao wana mama wabaya. Wanachotaka kufanya ni kupumzika na kutofanya kazi yoyote. Hawataki kuwa wakulima, hawataki kwenda shule, hawataki kufanya chochote lakini wanataka kujifurahisha. Walifurahi tu wakati wa likizo, mapumziko, mashindano ya michezo au sikukuu za kitaifa kwa maana hawakuwa na masomo.

Maudhui

hariri

Katika Ndoto ya Amerika kuna maudhui nyingi kama:

  1. Umaskini
  2. Chuki kwa nyumba yao
  3. Kutaka kuondoka/ Kutoroka
  4. Migogoro
  5. Ndoto
  6. Kifo
  7. Matumaini
  8. Umuhimu wa kutii wazazi
  9. Umuhimu wa elimu

Migogoro katika kitabu hiki inaonekana katika sura mbili za kwanza. Mama Isaya ni mtu mkali sana. Anaonyesha hisia zake kupitia migogoro. Unaweza kuona maudhui hii wakati Isaya analia na Mama Isaya anampiga kwa sababu alilia. Maudhui ya migogoro inaendelea wakati Isaya na Madoa wanakamatwa na polisi baadaye kwenye kitabu.

Kutoroka ni maudhui mkubwa pia. Tunaona Isaya na Madoa wanataka kutoroka makwao na kutoroka kenya. Isaya kutaka kuota kuhusu Marekani ili kuweza kutoroka kiakili. Msitu kupitia kitabu hiki ni muhimu sana. Msitu unawakilisha matumaini mapya. Japokuwa msituni ni mahali panapotisha na penye hatari nyingi kama wanyama wakali na nyoka, ni mahali salama kwa Isaya na Madoa kutorokea. Isaya na Madoa wanataka kuondoka nyumbani na kuacha shule zao lakini Madoa pia anataka kuondoka Afrika. Madoa hata anasema kila mtu ana ndoto ya kuondoka na kwenda Marekani.

Ndoto ni muhimu sana katika kitabu hiki. Maudhui hii inatuonyesha jinsi mtu anavyopaswa kujua namna kufikiri. Kuota Amerika kwenye kitabu ni kitu muhimu sana. Msomaji anajifunza kwamba kila mtu anakuwa na ndoto ya Amerika. Kuwa na ndoto hii kunaonyesha kuwa unataka mafanikio katika maisha yako. Hii huleta swali muhimu, je, ni lazima uondoke nyumbani kwako ili ufurahie maisha kweli?

Wahusika

hariri
  • Isaya Yano
  • Mama Isaya
  • Madoa
  • Mzee Zakayo Wekesa
  • Rock Mwamba
  • Hakimu

Marejeo

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Ken Walibora". www.goodreads.com. Iliwekwa mnamo 2022-04-21.
  2. https://www.the-star.co.ke/authors/current-affairs-reporter. "Ken Walibora: Life and times of renowned author". The Star (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-21. {{cite web}}: External link in |author= (help)
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndoto ya Amerika kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.