Nge-maji

(Elekezwa kutoka Nepidae)
Nge-maji
Nge-maji kahawianyekundu (Laccotrephes fuscus)
Nge-maji kahawianyekundu (Laccotrephes fuscus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo kama wadudu, nge, buibui)
Nusufaila: Hexapoda (Arithropodi wenye miguu sita)
(bila tabaka): Dicondylia (Wadudu walio na mandibula zenye condyle mbili)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Nusungeli: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda ya juu: Paraneoptera
Oda: Hemiptera
Haeckel, 1896
Nusuoda: Heteroptera
Oda ya chini: Nepomorpha
Familia ya juu: Nepoidea
Familia: Nepidae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusufamilia 2 na jenasi 14:

Nge-maji ni wadudu wa familia Nepidae katika oda ya chini Nepomorpha ya oda Hemiptera na nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Wanafanana na nge kwa sababu ya miguu yao ya mbele yenye nguvu na mkia mrefu (bila tezi ya sumu) ambayo kwa kweli ni mrija wa kupumua. Wadudu hao huishi ndani ya maji. Spishi za nusufamilia Ranatrinae huitwa wadudu-sindano pia.

Maelezo

hariri

Nge-maji ni wadudu kahawia ingawa wachache ni weusi au kijivu na spishi nyingine zina fumbatio nyekundu kali ambayo inaweza kuonekana wakati mabawa yamefunguliwa. Mwili wao ni mpana na bapa (nusufamilia Nepinae) au mrefu na mwembamba (nusufamilia Ranatrinae). Hawaogelei vizuri sana na kwa kawaida hutambaa juu ya mimea ya majini. Wanaweza kuruka angani, lakini hii inaonekana mara chache tu. Kwa takriban spishi zote urefu wa mwili ni kati ya sm 1.5 na 4.5, ingawa zile kubwa kabisa, kama Ranatra chinensis wa Asia ya Mashariki na R. magna wa Amerika ya Kusini, zinaweza kukaribia sm 6.

Upumuaji kwa wapevu hupatikana kwa njia ya mrija wa kupumua kwenye fumbatio, ambao una jozi ya nusu-mirija inayoweza kufungwa pamoja ili kuunda mrija mzima. Hewa inafyonzwa kupitia hiyo kuelekea makoromeo kwenye ncha ya fumbatio wakati ncha ya mrija inasukumwa juu ya uso wa maji (sawa na kipumulio au snorkel). Kwa spishi fulani mrija ni mrefu kuliko mwili, lakini kwa nyingine ni mfupi zaidi, kwa chache hata chini ya moja kwa kumi ya urefu wa mwili. Kwa hatua za kichanga mrija haujakua vizuri mara nyingi na upumuaji hufanyika kupitia jozi sita za matunduhewa kwenye fumbatio.

Miguu yao ya mbele imebadilika kuwa viungo vya kimbuai ambavyo hutumiwa kukamata mbuawa wao. Wadudu hao hujilisha hasa kwa invertebrata wa majini kama vile wadudu wengine, lakini mara kwa mara huchukua samaki wadogo au viluwiluwi. Mayai, yanayotagwa juu ya usawa wa maji katika matope, mimea inayooza, mashina ya mimea au mbao zinazooza, hutolewa kwa hewa kupitia matokezo kama nyuzi ambayo hutofautiana kwa idadi baina ya jenasi.

Ingawa nge-maji hawaumi kwa mkia wao, kung'ata kwao kuna uchungu (kusema ukweli ni kuumwa kwa mdomo wenye ncha kali), lakini hii haina madhara sana kwa wanadamu kuliko kuumwa na nge wa kweli.

Spishi za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Borborophilus afzelii
  • Laccotrephes annulipes check
  • Laccotrephes ater
  • Laccotrephes breddini
  • Laccotrephes calcaratus
  • Laccotrephes dissimulatus
  • Laccotrephes ellipticus
  • Laccotrephes fabricii
  • Laccotrephes fuscus
  • Laccotrephes gomai
  • Laccotrephes vicinus
  • Paranepa primitiva
  • Ranatra cinnamomea
  • Ranatra denticulipes
  • Ranatra fuscoannulata
  • Ranatra grandocula
  • Ranatra nodiceps
  • Ranatra parvipes
  • Ranatra varicolor
  • Ranatra vicina