Mfumo wa neva
Mfumo wa neva ni sehemu ya mwili wa wanyama ambayo inaratibu matendo yake ya hiari na yasiyo ya hiari na kutuma taarifa kati ya viungo mbalimbali.
Kwa mara ya kwanza tishu za neva zilitokea katika wadudu wa jamii ya minyoo (Ediacara biota) miaka milioni 550 hadi 600 hivi iliyopita.
Spishi nyingi za wanyama zina sehemu kuu mbili, sehemu ya kati ya neva na sehemu ya pembeni. Sehemu ya kati ya neva inajumuisha ubongo na mrija wa uti wa mgongo na sehemu ya pembeni inajumuisha neva zilizofungwa kwenye kambabando zilizounganishwa kwenye sehemu ya kati ya neva na sehemu nyingine za mwili.Sehemu ya kati ya neva hupeleka taarifa kutoka kwenye chanzo cha taarifa kupitia uti wa mgongo mpaka kwenye neva za ubongo. Pia sehemu nyingine za mwili zina neva ambazo hupeleka taarifa.
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mfumo wa neva kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |