Nyanya chungu

(Elekezwa kutoka Ngogwe)

Nyanya chungu (pia ngogwe au nyanyamshumaa) ni tunda la mngogwe, jamii ya mbiringani, ambalo linatumika kama mboga.

Ngogwe Habeshi
Ngogwe za Afrika

Ina wingi wa vitamini (A, B, C, K) na madini, hivyo inasaidia sana afya.

Ina ladha chunguchungu na huliwa kwa ugali, lakini ngogwe Habeshi inaweza kuliwa mbichi pia.

Mboga ya nyanya chungu wakati wa kupikwa huwekwa vitu vifuatavyo kama: nyanya, kitunguu, karoti na pilipili hoho, lakini pia bamia.

Jinsi ya kupika

hariri

Unawasha moto wako au gesi yako; ukishamaliza unaweka sufuria yako kwenye jiko na unaacha ipate moto kidogo. Ikishapata moto unaweka mafuta, unaacha yapate moto, halafu unaweka kitunguu. Ukishaweka unaacha mpaka kiwe cha kahawia. Kikishaiva unaweka pilipili hoho, ikishaiva unaweka karoti. Baada ya hapo unaacha vichemke. Vikishachemka unaweka nyanya, unaacha mpaka ziive. Nyanya zikishaiva unaweka nyanya chungu zako, halafu unatia maji kidogo na unafunika ili zichemke.

  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyanya chungu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.