Nguta (pia:mbata) ni nyama ya nazi ambayo ni mbegu wa mnazi. Kwa lugha nyingi huitwa "copra" kutokana na neno la Kimalayalam kopra (കൊപ്ര) kwa ajili ya nguta.

Nguta inakaushwa kwenye jua

Nguta hutumiwa kwa kutengeneza mafuta ya kulika.

Mbegu kupasuliwa baada ya mavuno. Nusu zake zinakaushwa kwa jiko au chumba cha joto muda wa masaa 24. Baadaye nyama kavuu hutoka rahisi katika ganda. Nguta inasagwa na kukandamizwa na mafuuta kutolewa.

Mabaki ya nguta yanafaa kama chakula bora cha wanyama.

Uzalishaji

hariri

Uzalishaji wa Nguta (milioni ya tani)
Namba za 2003-2004'

Takwimu wa FAOSTAT (FAO)

Indonesia 15 630 29 % 15 650 29 %
Ufilipino 13 700 26 % 13 700 26 %
India 9 700 18 % 9 700 18 %
Brazil 2 851 5 % 2 960 6 %
Sri Lanka 1 850 3 % 1 900 4 %
Uthai 1 420 3 % 1 450 3 %
Mexiko 959 2 % 959 2 %
Vietnam 920 2 % 950 2 %
Malaysia 710 1 % 710 1 %
Papua Guinea Mpya 570 1 % 650 1 %
Nchi nyingine 4 929 9 % 4 974 9 %
Jumla 53 239 100 % 53 603 100 %