Njiri

(Elekezwa kutoka Nigrita)
Njiri
Dume la njiri utosi-kijivu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Passeroidea (Ndege kama shomoro)
Familia: Estrildidae (Ndege walio na mnasaba na mishigi)
Bonaparte, 1850
Ngazi za chini

Jenasi 3, spishi 10:

Njiri ni ndege wadogo wa jenasi Nesocharis, Nigrita na Parmoptila katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Wanafana na mishigi wenye rangi za nyeusi, kijivu na kahawia, pengine nyekundu au buluu. Hula wadudu, matunda madogo na mbegu. Tago lao ni tufe la manyasi, nyuzinyuzi na vigoga lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-6.

Spishi

hariri