Nikwata
Nikwata madoadoa (Hemidactylus brookii)
Nikwata madoadoa (Hemidactylus brookii)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Sauria (Mijusi)
Oda ya chini: Gekkota (Mijusi-kafiri)
Familia: Gekkonidae (Mijusi-kafiri wa kawaida)
Gray, 1825
Jenasi: Hemidactylus (Nikwata na mijusi-kafiri vidole-majani)
Oken, 1817
Ngazi za chini

Spishi 12 za nikwata:

Nikwata ni spishi za mijusi-kafiri katika jenasi Hemidactylus ya familia Gekkonidae. Wamepewa jina hili kwa sababu huishi katika nyumba za watu mara nyingi. Spishi nyingine za Hemidactylus huitwa mijusi-kafiri vidole-majani na hawa wanatokea porini au msituni.

Kama mijusi-kafiri takriban wote nikwata hawana kope na hulamba macho mara kwa mara kuzuia yasikauke. Hukiakia usiku wakikamata wadudu.

Chini ya mguu wa mjusi-kafiri inaonyesha lamela sambamba.

Nikwata, na spishi nyingine zote za Hemidactylus, wana vidole vyenye ncha zilizopanuka (vidole-majani). Ncha hizi za vidole zinashika uso wowote, hata nyuso laini. Kwa hivyo wanaweza kutembea bila shida kwa ukuta na dari na hata kioo.

Spishi hariri

Picha hariri

Marejeo hariri

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nikwata kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.