Noah Bennet
Noah Bennet, pia anajulikana kama mtu mwenye miwani ya rimu ya pembe (aka HRG) au kwa kifupi Mr. Bennet, ni jina la mhusika wa kipindi cha maigizo ya ubunifu wa kisayansi wa katika kituo cha televisheni cha NBC, Heroes. Uhusika umechezwa na Jack Coleman. Hapo awali uhusika huu ulikuwa wa kuonekana kwa mara moja-moja, lakini umekuwa uhusika wa kawaida kuanzia katika sehemu ya 11t.[1] Jina lake la kwanza halikutambulika hadi ilipofika katika kipengele cha "How to Stop an Exploding Man", sehemu ya mwisho ya msimu wa kwanza.
Noah Bennet | |
---|---|
muhusika wa Heroes | |
Jack Coleman kama Noah Bennet | |
Mwonekano wa kwanza | "Genesis" |
Mwonekano wa mwisho | "Brave New World" |
Imechezwa na | Jack Coleman |
Maelezo | |
Kazi yake | Kachero wa zamani wa kina Company |
Ndoa | Sandra Bennet (-mekufa 2009) Kate Bennet (mke kuanzia 1985) |
Watoto | Claire Bennet (binti wa kumlea/mlinzi wake) Lyle Bennet (mtoto wake) |
Uwezo | Hana (lakini ana-maarifa ya hali ya juu katika kudhibiti watu wenye vipawa) |
Muhtsari wa uhusika
haririKatika kuonekana kwa mara ya kwanza, Noah Bennet anaonekana kama mfanyabiashara wa kawaida ambaye anafanya kazi katika kampuni ya Primatech Paper Company na anaishi mjini Odessa, Texas, akiwa na mke na watoto wawili. Hata hivyo, na washirika wenzake wamekuwa wakisafiri kila pembe ya dunia wakiwasaka watu wenye vipawa na kuwazingua wale waliozawadiwa vipawa hivyo.
Bennet anadai kwamba anawasaidia namna ya kujifunza kutumia vipawa vyao, japokuwa vikumbusho vya mazungumzo ya awali baina ya Noah ma Thompson vinaonyesha kwamba kazi yake dhahiri ni ya kuzua maswali na mara kadha wa kadha yaweza kusababisha madhara au matatizo asiyokusudia. Katika kipengele kimoja, anajisikia faraja kuwa na maadili sio. Ingawa anajali sana familia yake na atafanya chochote kuilinda, utiifu wake katika kazi yake hauna kikomo, na mara zote huweka mbele kupita vitu vyote.
Marejeo
hariri- ↑ Schneider, Michael. "'Heroes' zeros in on its bad guy", Variety.com, 2006-10-23. Retrieved on 2006-10-27.
Viungo vya Nje
hariri- Interview: "Jack Coleman Feels That Heroes is Something Special" Archived 26 Mei 2007 at the Wayback Machine., MediaBlvd Magazine, 27 Februari 2007.