Noureddine Amrabat (alizaliwa 31 Machi 1987), ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa anaecheza kama mshambuliaji wa pembeni katika ligi kuu ya Ugiriki akicheza katika klabu iitwayo AEK Athens.

Nordin Amrabat

Mshambuliaji huyu aliwahi kukipiga katika timu ya taifa ya vijana ya Uholanzi, lakini aliwahi kuitwa mara moja katika timu ya wakubwa. Mnamo tarehe 1 oktoba mwaka 2009, Amrabat alitangaza uamuzi wake wa kuitumikia timu ya taifa ta Moroko ambapo aliitumikia katika mashindano mawili ya Kombe la Afrika na katika mashindano ya Olimpiki mnamo 2012.

Maisha ya awali

hariri

Mzaliwa wa Naarden, Uholanzi Kaskazini, Amrabat aliachiliwa kutoka klabu ya Ajax akiwa na umri wa miaka 13, baada ya kudhoofika kwa ukuaji kutokana na ugonjwa wa Osgood Schlatter. Baba yake alipendekeza Amrabat kutocheza katika soka la kulipwa wakati akisomea taaluma tofauti. Aliosha vyombo na kusafisha shule yake alipokuwa akiichezea SV Huizen huko Huizen. [1] Akiwa na umri wa miaka 17, alipanga kusomea Usimamizi, Uchumi na Sheria. [2]

Marejeo

hariri
  1. Huizen, S. V. "Home | S.V. Huizen". www.svhuizen.nl.
  2. "New Watford signing Nordin Amrabat reflects on his different route to becoming a professional footballer", Watford Observer, 25 January 2016. 
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nordin Amrabat kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.