Norman Michael Ledgin (Passaic, New Jersey, 15 Julai 1928 - Stanley, Overland Park, Kansas, 18 Juni 2019) alikuwa mwandishi wa vitabu na mwandishi wa habari kutoka Marekani [1] . Alijulikana kwa vitabu viwili vinavyohusiana na usonji, "Asperger's and Self-Esteem: Insight and Hope Through Famous Role Models" (2002) na "Diagnosing Jefferson: Evidence of a Condition that Guided His Beliefs, Behavior, and Personal Associations" (2000). Kitabu cha pili kinadai kwamba Thomas Jefferson alionyesha dalili za ugonjwa wa Asperger. Mnamo mwaka 2012 alikamilisha riwaya ya kihistoria "Sally of Monticello: Founding Mother", ambayo inasimulia hadithi ya mapenzi ya miaka 38 kati ya Thomas Jefferson na Sally Hemings. [2]

Marejeo

hariri
  1. "Obituary for Norman Michael Ledgin". Johnson County Funeral Chapel & Memorial Gardens (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-07-07.
  2. Source, Future Horizons, Inc., publisher, Arlington, TX
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Norm Ledgin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.