Noti (kizio)

Kwa matumizi tofauti ya neno hili tazama Noti (maana)

Noti (kutoka Kiingereza: knot) ni kizio cha kasi. Kifupi chake ni kt au kn. Hutumiwa kimataifa kwa kueleza mwendo wa meli na eropleni, lakini pia katika metorolojia. Si kipimo sanifu cha SI. [1]

UfafanuziEdit

Noti 1 inafafanuliwa kutaja mwendo wa maili ya baharini 1 kwa saa. Maili ya baharini ni sawa na mita 1852.

MatumiziEdit

Matumizi ya kizio hicho ni kutaja kasi ya chombo cha majini. Huko Marekani kinatumiwa pia kwa mwendo wa eropleni na kutaja kasi ya mwendo wa hewa, yaani upepo.

AsiliEdit

Maana ya "knot" ni fundo; zamani kasi ya jahazi ilipimwa kwa kutumia kamba ndefu iliyokuwa na mafundo mengi. Kamba hiyo ilifungwa kwa kipande cha ubao kilichotupwa baharini kikifuatwa na kamba. Baada ya kipindi maalumu (kilichopimwa kwa kutumia saa ya mchanga) kamba ilirudishwa na mafundo yalihesabiwa.

MarejeoEdit

Tovuti za NjeEdit