Number One Remix

(Elekezwa kutoka Number One)

"Number One Remix" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 6 Januari, 2014 kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz akimshirikisha Davido kutoka nchini Nigeria. Wimbo unatoka katika albamu ya A Boy From Tandale na wa kwanza kutolewa kama single kutoka katika albamu hiyo. Huu ndio wimbo wa kwanza wa Chibu kuimba na msanii kutoka nchi za nje, halkadhalika kutoka nchini Nigeria. Wimbo unafungua njia mpya ya mahusiano ya kisanii kati ya Wanigeria na Watanzania. Kabla ya hapa, Chibu hakuwahi kufanya kazi na msanii yeyote yule kutoka Nigeria. Huu ulikuwa mwanzo mzuri kwa kazi za baadaye za Chibu.[1][2]

“Number One Remix”
“Number One Remix” cover
Kava ya Number One Remix
Single ya Diamond Platnumz na Davido
kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale
Imetolewa 6 Januari, 2014
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2014
Aina Bongo Flava
Urefu 3:26
Studio Burn Records
Mtunzi Diamond Platnumz
Davido
Mtayarishaji Sheddy Clever
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz na Davido
"Kesho"
"(2012)"
"Number One Remix"
"(2014)"
"Mdogo Mdogo"
(2014)

Wimbo huu umetayarishwa na Sheddy Clever kupitia Burn Records. Toleo halisi lilitoka tarehe 2 Septemba, 2013 na video kufanywa nchini Kenya chini ya Ogopa Videos - ambao hao ndio waliofanya video ya "Kesho". Video ya remix iliongozwa na Clarence Peters chini ya "Capital Dreams Pictures" ya nchini Nigeria. Chibu amefanya video moja tu na Capital Dreams, 2 na Ogopa Videos (Kesho na Number One halisi), 2 na Moe Mussa (Bum-Bum na Hallelujah), 7 na Godfather (Mdogo Mdogo, Ntampata Wapi, Nana, Utanipenda, Kwetu na Make Me Sing) halafu wengine kina Gbenga Sesan (Eneka), Kenny (Sikomi), Nicorux (Salome, Bado, Kokoro, Aiyola na nyenginezo).

Tazama pia hariri

Marejeo hariri