Taa (samaki)

(Elekezwa kutoka Nyenga)
Taa
Karwe (Manta birostris)
Karwe (Manta birostris)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Chondrichthyes (Samaki wenye gegedu)
Nusungeli: Elasmobranchii (Papa na taa)
Oda ya juu: Batoidea (Taa)
Ngazi za chini

Oda 4

Taa ni aina za samaki zilizo na mnasaba na papa. Papa upanga na papa charawanza ni aina za taa pia. Majina mengine ya samaki hawa ni shepwa, karwe , (ki)pungu na nyenga. Kama papa, taa wana kiunzi cha gegedu. Mwili wao ni bapa, isipokuwa ule wa papa upanga na papa charawanza, na mapefu yamekuwa mapana na kama mabawa. Hawana pezi la mkundu. Mdomo upo upande wa chini wa kichwa na hata matamvua yapo chini ya mwili kando ya mapefu. Takriban spishi zote zina jozi 5 za matamvua, lakini spishi kadhaa zinazo 6. Macho ya taa yapo juu ya kichwa na nyuma ya kila jicho kuna spirakuli moja. Taa wengi huvuta maji kupitia spirakuli na huyapitisha kwa matamvua ambayo hufyonza oksijeni kutoka maji haya. Mkia wa taa ni mrefu na mwembamba na hubeba msumari katika spishi nyingi.

Ingawa papa upanga ni aina za taa, wanafanana zaidi na papa wa kawaida, isipokuwa mwili wao ni bapa zaidi. Pua ni ndefu sana na inabeba meno kwa pande mbili zote. Pua hii hutumika kwa kukamata na kukata mawindo.

Papa charawanza, papa kiharere na papa wame ni aina za taa pia lakini wana mkia kama papa wa kawaida. Kichwa pamoja na mapefu ina umbo wa pembetatu au gitaa (kwa hivyo jina la Kiingereza: Guitarfish).

Spishi za Afrika ya Mashariki

hariri

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.