Nyigu-mahameli
Jike la nyigu-mahameli (Dasymutilla occidentalis)
Jike la nyigu-mahameli (Dasymutilla occidentalis)
Dume la nyigu-mahameli (Dasymutilla occidentalis)
Dume la nyigu-mahameli (Dasymutilla occidentalis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno kipana)
Familia ya juu: Pompiloidea
Familia: Mutillidae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusufamilia 8:

Nyigu-mahameli au sisimizi-mahameli (kutoka kwa Kiing. velvet ants) ni nyigu wadogo wa familia Mutillidae katika nusuoda Apocrita ya oda Hymenoptera ambao majike wao wanafanana na sisimizi wakubwa. Wana nywele nyingi kama mahameli mara nyingi zenye rangi kali kama nyekundu, machungwa au njano.

Maelezo

hariri

Majike huanzia kwa ukubwa kutoka mm 6 hadi 20, madume ni wakubwa zaidi. Majike hawana mabawa na hufanana na sisimizi, lakini madume wana mabawa na hufanana na nyigu wengine. Spishi nyingi zina nywele za rangi, kwa kawaida nyekundu, machungwa au njano, ingawa baadhi wana nywele nyeupe au fedha au ni weusi kabisa. Madume hawana rangi nyingi. Kiunzi nje ni kigumu sana, ambayo k.m. hufanya iwe vigumu kwa wana-entomolojia kubandika vielelezo. Hulinda nyigu wanapoingia kwenye viota vya mbuawa wao, na huwasaidia kuhifadhi unyevu. Mara nyingi sana, madume na majike ni tofauti sana kiasi kwamba ni vigumu kujua ikiwa ni spishi moja au tofauti. Kwa kisa hicho, inapaswa kuwaangalia wakati wa kupandana. Katika spishi kadhaa, madume huruka huku wakiwa wameshikilia majike kwenye miguu yao.

Majike wana neli ya kutagia iliyorekebishwa ambayo hutumika kuwachoma washambuliaji. Mchomo unaleta uchungu kali sana, lakini sumu siyo kali kama ile ya nyuki-asali. Kwa bahati nzuri nyigu hawa hawana fujo na huchoma tu wakati wa kushikwa kwa mkono. Jinsia zote mbili zina muundo maalum juu ya fumbatio ambao hutumiwa kutoa sauti nyembamba au ya mlio wakati wa kutishwa.

Biolojia

hariri

Madume wa nyigu-mahameli huruka huku na huko kutafuta majike. Baada ya kupandana jike huingia kwenye kiota cha mdusiwa, kwa kawaida nyuki au nyigu anayejenga viota ardhini, na kuweka yai moja kando ya kila buu au bundo. Mabuu wanaoibuka kisha hukua kama vidusia wa nje na hatimaye kuua mbuawa wao.

Spishi za Afrika ya Mashariki

hariri
  • Barymutilla parallela
  • Barymutilla pythia
  • Ceratotilla dolosa
  • Ceratotilla obtusa
  • Ceratotilla shiratiana
  • Dasylabris deckeni
  • Dasylabris foxi
  • Dasylabris signaticeps
  • Dasylabris somalica
  • Dentotilla crassa
  • Dentotilla mpandaana
  • Dentotilla pavesii
  • Dolichomutilla langenburgensis
  • Dolichomutilla sycorax
  • Glossotilla casignete
  • Labidomilla langi
  • Mutilla astarte
  • Mutilla dasya
  • Mutilla dentidorsis
  • Mutilla diselena
  • Mutilla fulvodecorata
  • Mutilla parallaela
  • Mutilla penetrata
  • Mutilla tegularis
  • Mutilla triodon
  • Mutilla vetustata
  • Odontomutilla argenteoguttata
  • Odontomutilla inversa
  • Odontotilla bidentata
  • Odontotilla fasciata
  • Odontotilla tridentata
  • Omotilla conjuncta
  • Omotilla conjunctoides
  • Omotilla graziani
  • Pristomutilla ctenothoracica
  • Smicromyrme bayeri
  • Spinulomutilla argenteiventris
  • Spinulomutilla frater
  • Spinulomutilla kifaruana
  • Spinulomutilla pseudopygidialis
  • Spinulomutilla quadrituberculata
  • Trogaspidia medonopsis
  • Trogaspidia panganina
  • Tropidotilla milmili
  • Tricholabiodes pedunculatoides
  • Tuberocoxatilla lingulata