Nyigu-msumeno
Nyigu-msumeno | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Arge humeralis
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Familia za juu 6; 4 na familia 5 katika Afrika:
|
Nyigu-msumeno (kutoka kwa Kiing. sawflies) ni wadudu wa nusuoda Symphyta katika oda Hymenoptera walio na mrija wa kutagia mayai ufananano na msumeno. Hawana kiuno chembamba sana kama nyigu wa kawaida. Spishi za familia Siricidae huitwa nyigu-ubao pia na zile za Orussidae ni vidusia wa lava wa mbawakawa na nyigu ambao huishi ndani ya ubao wa miti. Nusuoda hii ina takriban spishi 8000 duniani kote na zaidi ya 90 katika Afrika ya Mashariki.
Maelezo
haririNyigu-msumeno wengi sana wana urefu wa mm 2.5-20, ingawa wengine wanaweza kufikia mm 55. Wanafanana na nyigu wa kweli kwa kiasi fulani, lakini hawana kiuno chembamba cha hao[1]. Mrija wao wa kutagia ni kama msumeno ili kukata ndani ya tishu za mimea. Baadhi ya nyigu-msumeno huiga nyigu au nyuki ili kupunguza uwindaji na mrija wao wa kutagia unaonekana kama mwiba.
Majike hutumia mrija wa kutagia kama msumeno ili kukata ndani ya bua la mmea au shina la mti na kutaga mayai. Lava wanaonekana kama viwavi lakini wana miguu ya bandia zaidi, ambayo pia haina ndoano. Wengi sana hula majani huku wengine wakila ndani za mabua ya mimea. Lava wa Siricidae hula ubao na wale wa Orussidae hula mabuu ya mbawakawa na nyigu wanaokula ubao. Lava wanaoishi huru hula mara nyingi katika makundi mazito ili kuzuia uwindaji.
Wapevu wa nyigu-msumeno huishi siku 7-9 tu, lakini lava wanaweza kudumu kutoka miezi hadi miaka kadhaa kulingana na spishi. Majike wengi wanaweza kutaga mayai yanayoendelea bila madume, yaani wao ni pathenojenetiki. Hata hivyo, spishi nyingine nyingi bado zina madume. Wapevu hula mbelewele, mbochi, mana ya wadudu, utomvu au hemolimfu ya wadudu wengine.
Baadhi ya spishi, kama vile nyigu-msumeno wa misonobari, zinaweza kusababisha hasara kubwa wakati idadi ya wadudu inakua kubwa sana, kwa kutoa majani ya miti na kusababisha kudumaa kwa ukuaji na hata kifo[2]. Hata hivyo, kwa ujumla, nyigu-msumeno wana umuhimu mdogo wa kiuchumi.
Spishi za Afrika ya Mashariki
hariri
|
|
|
Picha
hariri-
Cephidae (nyigu-bua Cephus spinipes)
-
Orussidae (nyigu-ubao kidusia Guiglia schauinslandi katika ubao)
-
Siricidae (nyigu-ubao Sirex nigricornis)
Marejeo
hariri- ↑ Goulet, H.; Huber, J.T. (1993). Hymenoptera of the World: An Identification guide to families (PDF). Ottawa, Ontario: Agriculture Canada. ISBN 978-0-660-14933-2. Archived from the original (PDF) on 5 March 2016 https://web.archive.org/web/20160305012733/http://www.esc-sec.ca/aafcmonographs/hymenoptera_of_the_world.pdf.
- ↑ Krokene, Paal (6 December 2014). "The common pine sawfly – a troublesome relative". Science Nordic. Retrieved 28 November 2016.