Nyumba ya Chilenje 394

Nyumba ya Chilenje 394 ni makumbusho yanayopatikana katika eneo la Chilenje, Lusaka nchini Zambia.

Nyumba hiyo ilikuwa makazi ya Kenneth Kaunda aliyeishi hapo kuanzia Januari 1960 hadi Disemba 1962, na baadaye kuja kuwa rais wa kwanza wa nchi ya Zambia. Harakati za ukombozi wa uhuru nchini humo zilianzia katika nyumba hiyo hadi mafanikio ya taifa huru yalipopatikana tarehe 24 Oktoba 1964.[1]

Ni nyumba iliyogawanyika katika vyumba viwili vya kulala, sebule ndogo pamoja na jiko. Ni nyumba inayopatikana katika eneo ambalo miti yake inaonekana kustawi vizuri[2]

Tazama Pia hariri

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyumba ya Chilenje 394 kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.