Ogaden
Ogaden ni jina la kimataifa la eneo kubwa la Ethiopia ya mashariki. Zamani ilikuwa jina la jimbo linaloitwa leo Jimbo la Somali la Ethiopia.
Ogaden imepakana na Kenya, Somalia na Jibuti.
Eneo hili lina umbo la pembetatu na jumla ni takriban kilomita za mraba 370,000. Hali ya hewa ni yabisi, kuna sehemu ambazo ni jangwa kabisa, nyinginezo savana yabisi.
Kwa miaka mingi vikundi vya wanamgambo wamejaribu kutenganisha eneo hili na Ethiopia lakini hawakufaulu. Miaka 1977-1978 kulitokea Vita ya Ogaden ambamo jeshi la Somalia lilijaribu kuteka eneo hili kwa msaada wa wanamgambo wenyeji. Hatimaye walishindwa na Waethiopia kwa msaada wa Warusi na Wakuba.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ogaden kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |